Thursday, August 22, 2013

TUNATEGEMEANA KATIKA MAISHA YETU


Maisha yetu ya kila siku tunategemeana kwa kila kitu. Ni kama huyo mama hapo pichani ili asonge ugali wake vizuri anatumia zana maalumu (kwetu tunaita mpanti) ili sufuria lisimsumbue wakati anapika ugali wake, na uive vizuri. 

Napenda niwatakie kazi/shughuli njema popote mlipo, tutegemeane kwa nia njema kabisa katika shughuli zetu ili kuongeza ufanisi na kipato pia.

Tuesday, August 20, 2013

BAADHI YA VYAKULA VIFAAVYO BAADA YA KUJIFUNGUA AMBAVYO NILIVIFURAHIA NA KUVILA SANAAAAAAA

 Uji 
 Supu ya Nyama ya Ng'ombe
 Mtori
Ndizi laini

Hivyo ni baadhi tu, kwani katika maisha yangu yote sikuwahi kuupenda mtori, nadhani nilikuwa napikiwa sivyo, ila wa sasa hivi Mama mkwe aliokuwa ananipikia niliupenda sana hadi leo hii ukinipa mtori naufurahia, ulikuwa unapikwa vizuri, siku nyingine anaweka samaki..........nimekuwa Member mzuri sasa wa huu msosi.

HAYA MASHAVU NILIYONAYO HAYAJAJA HIVI HIVI, MTORI UNATUGAWIA AFYA NJEMA YA MIMI NA BABY ALVIN

SIKU NJEMA WAPENDWA

Monday, August 19, 2013

NIMEWAKUMBUKA SANA WAPENDWA WANGU

Habari ya siku nyingi wapendwa? Mwaendeleaje? 

Samahani sana kwa ukimya wa gafla uliokuwa umetokea, kwani nilikuwa busy kupokea Ugeni uliokuwa umetufikia nyumbani kwetu ambao ulisababisha nipotee gafla mahala hapa. 


Tunamshukuru Mungu tumejaaliwa kupata mtoto wa kiume aitwaye ALVIN, na sasa Likizo/mapumziko ya muda yameisha nitakuwa nanyi mezani hapa tuelimishane na kubburudishana kama ilivyokuwa ada yetu.


Sunday, May 12, 2013

HERI YA SIKU YA AKINA MAMA DUNIANI: AKINA MAMA WOTE OYEEEEEEEE

Mama anatakiwa apewe heshima zake zoooooote, analisha wanae wawili kwa pamoja na bado ana tabasamu zuri usoni kwake, huu ni upendo wa hali ya juu alionao
Mama anatakiwa asaidiwe pia kwenye majukumu mbali mbali na hili ni moja wapo
Mama huwa yuko tayari kuhakikisha familia yake inakula, hata kama ni kidogo wale kwanza watoto yeye baadae, kikiwa kingi ni furaha kwake kuwa familia yake itashiba vema na kupata afya
Mama anastahili apewe Busu takatifu kama hili ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo kwake na kuthamini ayafanyayo katika jamii

AKINA MAMA WOOOOOTE NAWATHAMINI SANA NA KUWAPENDA MNO, MUNGU NAOMBA UNIBARIKI NIWE MAMA BORA NA MWEMA NIWEZE KUITUNZA FAMILIA YANGU VEMA NA KUITHAMINI JAMII INAYONIZUNGUKA......AMEN

Tuesday, May 7, 2013

TIKETI ZA SHOW YA JAYDEE: KAJIPATIE YAKO MAPEMAAAAAAAAAA

Tiketi za sherehe za kuadhimisha miaka 13 ya muziki wa Lady Jaydee zimeshaanza kuuzwa mtaani na huo hapo juu na chini ndio mfano wa jinsi zilivyo ambapo ya juu ni ile ya VIP itakayokuwezesha kupata chakula, nakala ya CD pamoja na huduma maalum ya kinywaji cha kuanzia
Hii hapa chini ni ya kawaida itakayokuwezesha kushiriki onesho, na kushuhudia burudani lukuki zitakazoongizwa na Profesa Jay, TID, Matonya, Grace Matata pamoja na Lady Jaydee mwenyewe na Machozi Band itaonekana jukwaani live siku hiyo.
Tiketi zinapatikaka Shear Illusions-Mlimani City, BM BarberShops-Kinondoni, City Sports Lounge-City Centre, American Nails-Kinondoni, Nyumbani Lounge-Tranic Plaza, na katika Bar za Samaki samaki

Thursday, May 2, 2013

HII SHOW SIYO YA KUKOSA KABISAAAAAAAAAA


VYA KWETU TUVIKUMBATIE, VYA KWAO TUWAACHE WANAHANGAIKA NAVYO

NI PALE PALE NYUMBANI LOUNGE, JIDE ATAZIDI KUUWASHA MOTOOOOOOOOOOO

JOIN NOW AT SILVA INSTITUTE OF BUSINESS AND MANAGEMENT

ABOUT SIBM
Silva Institute of Business and Management (SIBM) was the registered on 4th April 2013 under the Business Names (Registration) Act (Cap 213). CIBM is owned by BluWat Tanzania Limited (BW), a limited liability company incorporated in Tanzania under the Companies Act, 2002 vide Certificate of Incorporation number 86598 issued on 20th October 2011. BluWat Tanzania Limited has the Consultancy licence; it consults mainly in Management and Business Services.
Vision
To become a centre of excellence in knowledge and technological advancement in East Africa thereby providing lifelong learning and superlative quality education Mission To function as knowledge and technological centre by
Continuously investing in the capacity building of the institute management, staff and infrastructure
Building reputation in the quality of education offered to satisfy the needs of eventual employers of the graduates and to suit the social and economic development needs.
Conducting research and development studies that will enable the institute to become the most trusted centre in provision of professional advice in economics and business management.
PROGRAMS OFFERED
Basic Technician Certificate In Procurement And Logistics Management (BTCPLM)
Basic Technician Certificate In Accoutancy (BTCA)
Basic Technician Certificate In Human Resource Management (BCHRM)
Basic Technician Certificate In Business Administration (BTCBA)
Front side.
REQUIREMENTS
Qualified selected applicants will be informed by admission letters before course commencement. Each student will be required to have four (4) passport size photographs (colour) for processing of identity card and other official uses. Identity Cards will be available immediately after completing registration at the institute. All students will therefore be required to submit a satisfactory Medical Examination report from a recognized Health Facility dully filled, signed and stamped by a qualified Licensed or registered Medical Practitioner.
The Foundation course is open to form four leavers who were not able to secure at least three principal passes at level (D) hence ineligible to join Basic Technician certificate programme.
Candidates for the Basic Technician courses should have attained certificate of secondary school education with a minimum of 3 passes at level (D) of the major subjects.
Candidates for the Technician courses should have attained a Basic Technician certificate from a recognised college.
Candidates for the ordinary diploma courses should have completed advanced level education with at least two principal passes or a Technician certificate from a recognised college on the respective course.
Inside class room.
CONTACTS
The college is located at Plot No 90, Block D, Kimbiji, Kijaka, Kigamboni in Temeke district. Administratively, Temeke is divided into three divisions namely Chang’ombe, Mbagala and Kigamboni. Kigamboni is situated in Dar-Es-Salaam, Tanzania and its geographical coordinates are 6° 49' 0" South, 39° 19' 0" East. According to various studies, the presence of unpolluted beaches, the redevelopment of Kigamboni will spearhead economic development and increase the national income.
The Principal,
Silva Institute of Business and Management,
P. O. Box 15805,

USAFI NA USALAMA WA CHAKULA NA MAJI: SEHEMU YA TATU

Usafi wa sehemu ya kutayarishia chakula


1. Hakikisha jiko au sehemu ya kutayarishia chakula ni safi.

2. Kusanya uchafu na mabaki ya vyakula na kuyatupa kwenye shimo la taka au kwenye chombo kilichofunikwa.



Monday, April 29, 2013

LEO TWENDENI MOROGORO TUKAMTEMBELEE AFANDE SELE

 Ilikuwa siku ya birthday yake....Afande Sele akiwa na rafiki zake wakichoma vichomwavyo
Hahahahaha kama anasema 'nipe hiyo nionje kama imeiva' sai sana

NAWATAKIA JUMATATU NJEMA WOTE