Thursday, May 17, 2012

NAMNA YA KUPIKA DAGAA+NYANYA CHUNGU+NAZI: RURAL OR URBAN STYLE

Hawa ni wale dagaa wa kigoma lakini wadogo wadogo sana, wachambue vizuri kwa kiasi utakacho kupika, halafu uwaoshe vizurii wasiwe na michanga
Andaa kitunguu, nyanya, carrot, hoho, ndimu na nyanya chungu, bila kusahau tui la nazi
 Weka mafuta kidogo sana kwenye sufuria kwakuwa mboga yetu tunaweka nazi, yakipata moto weka dagaa zako ulizozisafisha vizuri, zigeuze geuze halafu weka maji ya ndimu uliyokamua, geuza geuza moto usiwe mkali sana, katia kitunguu, endelea kugeuza hadi uone vitunguu vinageuka rangi na kuwa brown, halafu weka nyanya ulizokatakata ukachanganya na hoho na carrot, funika kwa muda kidogo inategemea na wingi wa mboga yako, ukifunua nyanya zitaanza kulainika ukigeuza utaona zinachanganyika na dagaa kuashilia zinalainika
Kabla hazijalainika sana, weka nyanyachungu kwa juu ulizokatakata ukubwa uutakao, kwakuwa nyanya  huwa zina maji mpaka hapo unakuwa hujaweka maji, ila ukiona mboga inashika chini, weka maji kidogo, funika, baada ya muda funua geuza geuza, weka chumvi kiasi, yale maji yakianza kukauka na kwakuwa nyanyachungu hazitakiwi ziive sana na kulainika sana weka tui lako
 Ukiweka tui la nazi acha ichemke vizuri, chumvi iwe ya kutosha isizidi sana maana chumvi ikizidi ni matatizo, utakuwa umeridhika imeiva ipua
 Na hii ni mboga yetu ikiwa tayari kuliwa na wali, ugali, ndizi za kuchemsha, mihogo ya kuchemsha, viazi hali kadhalika, ni tamu sana
Ukishakula, baada ya nusu saa, shushia matunda yako bila kusahau maji ya kunywa, unamshukuru Mungu kwakukujalia msosi kama huu, unawaza next meal itakuwa ni chakula gani.

Msosi huu umeangalia mtu wa kawaida kabisa na aishiye mazingira yeyote either mjini au kijijini na mahali ipatikanapo nazi, na ni mboga ya kupika kwa muda mfupi sana,mpishi ni mimi mwenyewe

ENJOY

9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ester nakuja yaani usimaliza kabisa nipo njiani...

Ester Ulaya said...

Yasinta karibu sana my dear

Yasinta Ngonyani said...

Ester unajua kama mie nahitaji ugali mkubwa kweli kwa hiyo ukiandaa kidogo utakuwa hujanifania jema:-) Maana hao Dagaa nazi wanaonekana watamu kwelikweli.

Ester Ulaya said...

hahahaha hata ukisema nisonge debe kwa wewe wala usijali nitafanya hivyo, na wingi wa mboga nitaongeza

Majoy said...

DUH ACHA NINYE MAJI MAANA NIMESHIBA MATE LOL!! TAMU SANA HIYO INAONEKANA ULI-ENJOY SANA.

Majoy said...

hahahahaaa sikuona hiityping error jamani doh eti ninye maji badala ya ninywe maji!!

Ester Ulaya said...

hahahahaha Majoyy nilikuwa sijaona hiyo mistake, nimechekajeee

ngaizaskids said...

Kitu cha my wii hicho chezea hapa kaka alete mahali ya pili, wii nitumie ems nijiwahi mie make mate yanandondoka hapa. Nkija ntabeba debe la dagaa vilivyobaki napata kwa wachina.

Ester Ulaya said...

My wii jiandae, utabeba hata gunia zimaaaaa