Tuesday, August 20, 2013

BAADHI YA VYAKULA VIFAAVYO BAADA YA KUJIFUNGUA AMBAVYO NILIVIFURAHIA NA KUVILA SANAAAAAAA

 Uji 
 Supu ya Nyama ya Ng'ombe
 Mtori
Ndizi laini

Hivyo ni baadhi tu, kwani katika maisha yangu yote sikuwahi kuupenda mtori, nadhani nilikuwa napikiwa sivyo, ila wa sasa hivi Mama mkwe aliokuwa ananipikia niliupenda sana hadi leo hii ukinipa mtori naufurahia, ulikuwa unapikwa vizuri, siku nyingine anaweka samaki..........nimekuwa Member mzuri sasa wa huu msosi.

HAYA MASHAVU NILIYONAYO HAYAJAJA HIVI HIVI, MTORI UNATUGAWIA AFYA NJEMA YA MIMI NA BABY ALVIN

SIKU NJEMA WAPENDWA

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Twafurahi kusikia mna afya njema wote mama na mtoto. Endelea kuvila ili maziwa yawe ya kutosha kwa mtoto Alvin.

Ester Ulaya said...

Asante sana dada, nitaendelea kufanya hivyo

Rachel siwa Isaac said...

Duuhh umefauduuu..huu uji wa nini? Napata picha umenenepa sana..Jichane mama Alvin..Kuzaa raha kama unamtu wa kukutunza/kukuangalia!!!

Ester Ulaya said...

Rachel mpenzi huo ni uji wa mahindi umewekwa blue band na pili pili manga

Cymah Wandelt said...

Wow my wii kwa raha zako, nakuoneaje gere sasa?? Supu ya matoke, nyanya chungu na utumbo umeonja? Uwiii sijui nikamilizie huko huko lol! Nakuonea raha my wii a kiss to my Alvin