Wednesday, April 10, 2013

LEO NI KUMBU KUMBU YA SIKU YA KUZALIWA YA MR. CATHBERT ANGELO


 Ikiwa leo ni kumbukumbu yako ya siku ya kuzaliwa, nakupongeza sana kwakuwa bado unapumua na una afya njema kabisa, endelea kufanya kazi kwa bidii pale unapokuwa na nafasi
 Jali afya yako bila kuisahau, kwani bila ulaji/unywaji mwili utayumba na hutaweza kutimiza majukumu yako
 Wewe ni mume bora sana, nafurahi na ninashukuru sana kwa matunzo unayoendelea kunipa hadi sasa, Mungu akubariki na akuongezee hekima zaidi, Upendo na afya njema ikiambatana na umri mrefu
Uwe kiongozi mzuri popote unapojikuta unatakiwa uwaongoze watu katika nyanja mbali mbali
NAKUPENDA SANA MUME WANGU.....ONE LOVE

Saturday, April 6, 2013

YANAYOJIRI BEACH KIDIMBWI KINONDONI BLOCK 41 - DAR

  Nikiwa na rafiki Beach Kidimbwi mida ya jioni baada ya kazini
 Marafiki tukipiga story za hapa na pale
 Hizi mvua zinazoendelea Dar zinasababisha madimbwi kujaa hasa ya barabarani......nasi chini ya miti hiyo huwa ni sehemu yetu ya kupumzika na kukutana na marafiki mbali mbali tukibadilishana mawazo....tukapaita Beach Kidimbwi
 Kuna kimvuli kizuri tu cha huo mti, kipindi cha kiangazi ni ukame na vumbi hasa magari yakipita kwa kasi
 Bajaji ikakwama hapo ikapata msaada kutoka kwa rafiki ikatolewa
 Mvua ikipamba moto napo panapamba moto maji kujaa
 Biashara ya nguo tukitembezewa na wamachinga
Biashara ya vitumbua ikiendelea nyakati za asubuhi

NAWATAKIA JUMAMOSI NJEMA YENYE AMANI....TUEPUKANE NA VURUGU ZISIZOTULETEA MAENDELEO

Friday, April 5, 2013

USAFI NA USALAMA WA CHAKULA NA MAJI: SEHEMU YA PILI

Usafi wa vyombo

1. Osha sawasawa vyombo vilivyotumika kutayarishia vyakula vibichi hasa nyama, samaki, au mayai kabla ya kuvitumia kutayarishia vyakula vingine.








2. Ni muhimu kuwa na kichanja cha kuanikia vyombo.








3. Hakikisha sehemu ya kuhifadhi vyombo ni safi na kavu

Sunday, March 31, 2013

NAWATAKIA PASAKA NJEMA NA YENYE AMANI

TUSALI

TULE

TUNYWE

TUWE NA FAMILA ZETU AU MARAFIKI ZETU HASA KUTAFAKARI MAANA YA HII SIKU NA KUSHEREHEKEA KWA AMANI


TWAWATAKIA PASAKA NJEMA..........ONE LOVE

Thursday, March 28, 2013

USAFI NA USALAMA WA CHAKULA NA MAJI: SEHEMU YA KWANZA


Usafi wa mtayarishaji wa chakula

1. Osha mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka na ya kutosha kabla ya kutayarisha chakula au baada ya kutoka chooni.


2. Hakikisha usafi wa mwili na nguo.


3. Funga vidonda vilivyoko kwenye mikono wakati wa kutayarisha chakula.


Nawatakia alhamisi njema, tukutane wakati mwingine

Wednesday, March 27, 2013

ANGELINA JOLIIE NDANI YA CONGO NA RWANDA: SURA ZA KIAFRIKA ZIKIONYESHA UNYONGE ZAIDI

 @ANzolo refugee camp




Laying down flowers: Angelina Jolie lay wreaths Gisozi genocide memorial in Kigali, the capital of Rwanda on Sunday 

Tuesday, March 26, 2013

LEKATUTIGITE: MIGEBUKA NA DAGAA WASAFI INAIPAMBA KIGOMA

 Kijiji pembezoni mwa ziwa Tanganyika....shughuli yao kuu ni Uvuvi

 Migebuka mtegoni
 Dagaa wabichi
 Dagaa wakianikwa mchangani

Dagaa zilizokauka Kwenye mifuko tayari kusafirishwa

Hii ndo Kigoma