Wednesday, September 19, 2012

SARANDA: SHERATON HOTEL ILIYOPO SINGIDA

Hapa ndo Saranda kuku wengi mnoooooo....wengine hadi wanataniaga kuwa hao siyo kuku ni Mwewe.....Mwewe gani ana paja kubwa hivi???????
 Maji yanazwa kwa kikombe
 Nyomi la haja.........moshi kuashiria kuna majiko yanafanya kazi
 Maji kikombe kimoja shilingi Mia 
 Biashara zikiendelea
 Mikooooooooooo
 Pia Waomba misaada wapo kama babu huyo

 Haya maaaji......haya maaji
 VYUKUUUUUUUUU
 WOTE KWENYE MSTARI....KUKU MZIMA WA KIENYEJI AMESHACHOMWA 5000/-
Babu ametengeneza kopo special na mti anaomba chochote kwakuwa Train ipo juu  hivyo mwenye chochote amdumbukizie humo

Tuesday, September 18, 2012

MPAKA CHINIII MPAKA CHINIIIIIIIII.........


Wacha weeeeeeeeee

DODOMA YETU ALONG RAILWAYBAADHI TU YA VIJIJI

 Station ya Dodoma Mjini.....train ilifika mida ya saa 2 asubuhi...wakashuka washukao...wakapanda wapandao....na tukashuka kuvuta pumzi na kuzunguka zunguka kidogo kabla safari kuendelea

 IDODOMYAAAAAAA
 Zao la Dodoma Wine.......tukauziwa tukabeba zawadi
Mabehewa ya Mizigo
 Vyumba vimepunguza mvuto, vitanda na mikanda yake imeishaaa......napenda kitanda cha juu na nilala hicho
 First Class ni ya Vitanda Viwili tuuuu....
 Juu na Chini ni Mnyororo jumla ya mabehewa 15 kama sikosei nilihesabu hivyo ukijumlisha na Engine/Kichwa yanakuwa 16

 Hiki kijiji kinaitwa Zuzu...sasa sielewi walikuwa na maana gani kukiita hivyo
Dodoma Inasifika kwa Ukame.....Check Ardhi Ilivyonuna

 Ubuyu na Ukwaju unapatikana kwa wingi Mkoa huu...ni mazao yanayostawi sana sehemu za Ukame...Hiki ni Kijiji Kingine
 Ndoo kama hii wanauza elfu mbili mia tano
 Kile paleeeeeeeeeee ni kisima cha maji cha kupump
 Asili yao Nyumba za Tembe
 Vikapu na Mifagio kwa wingi.............
Kofia za Kiasili kabisa zinauzwa....Hiki ni kijiji kingine tena baada ya Dododma Mjini
 Mtoto akifanya Biashara ya Mifagio akiwahi kwa style ya ki- Usain Bolt kupeleka kwa abiria kuwauzia 
Abiria wakiwahi Train iliposimama kwani kwenye vijiji kama hivi huwa inasimama kwa Dakika 2, zikizidi kunakuwa na shughuli isiyokwepeka........then inaendelea na safari
 Watoto wakifanya biashara ya ukwaju.......Mdau unaliongeleaje hili?
 Maskini huyu baba tulimuta kijiji kingine...inaonekana mzigo ulikuwa mzito...sasa kabla hajapanda na zile dakika 2 za Train kusimama ikaondoka kabla hajafanikiwa kupanda, ikamuacha duh
Babu akiwa busy akiuza Kofia

KIASILI ZAIDI






NILIKUWA BUSY NA SAFARI WAPENDWA - RELI YA KATI HII

 Safari ya kuelekea Tabora ilianzia hapa........Nilikuwa sijasafiri kitambo na Train....nilipoambiwa zimeanza upya nikaona nisafiri na usafiri huu ingawa bado haujaboreshwa sana......nili enjoy...kunesa kwa sana
 Haloooo....Ndiyo.....Ndo nataka nipande.....sawa....Asante sana
 Happy Wife......
 Nikiingiza Mizigo chumbani

 Nikichagua upi unifaao
 Gogo
 Namba ya Behewa nililopanda
Jembe alikuwa sambamba kumsindikiza dada....MSHUA HAONEKANI PICHANI, alikuwa msindikizaji pia

Keep refreshing the Page....More photos zaja

Sunday, September 16, 2012

MSAFARA WA MBIO ZA MWENGE WAPATA AJALI RUKWA, KADHAA WAJERUHIWA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI

Gari iliyokuwa imewabeba madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga katika msafara wa Mwenge ambayo ilipinduka jana katika kijiji cha Luwa na kujeruhi vibaya zaidi ya Madiwani watatu, hali iliyosababisha madiwani hao kukimbizwa hospitali ya mkoa mjini Sumbawanga. Picha na Mussa Mwangoka.
Mmoja kati ya madiwani wa Halmashauri ya Manispaa waliojeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa mjini Sumbawanga, akipata huduma ya kwanza baada ya kunusurika kwenye ajali ya gari walilokuwa wakilitumia katika msafara wa Mwenge ambayo ilipinduka jana asubuhi katika kijiji cha Luwa. hakuna mtu aliyefariki dunia katika ajali hiyo. Picha na Mussa Mwangoka.

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, HONEST MWANOSSA AKIPANDIKIZA SAMAKI KATIKA MMOJA YA MABWAWA YALIYOPO ENEO LA KANKWALE JANA BAADA YA KUZINDUA MRADI WA UFUGAJI SAMAKI