Sunday, September 16, 2012

MSAFARA WA MBIO ZA MWENGE WAPATA AJALI RUKWA, KADHAA WAJERUHIWA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI

Gari iliyokuwa imewabeba madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga katika msafara wa Mwenge ambayo ilipinduka jana katika kijiji cha Luwa na kujeruhi vibaya zaidi ya Madiwani watatu, hali iliyosababisha madiwani hao kukimbizwa hospitali ya mkoa mjini Sumbawanga. Picha na Mussa Mwangoka.
Mmoja kati ya madiwani wa Halmashauri ya Manispaa waliojeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa mjini Sumbawanga, akipata huduma ya kwanza baada ya kunusurika kwenye ajali ya gari walilokuwa wakilitumia katika msafara wa Mwenge ambayo ilipinduka jana asubuhi katika kijiji cha Luwa. hakuna mtu aliyefariki dunia katika ajali hiyo. Picha na Mussa Mwangoka.

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, HONEST MWANOSSA AKIPANDIKIZA SAMAKI KATIKA MMOJA YA MABWAWA YALIYOPO ENEO LA KANKWALE JANA BAADA YA KUZINDUA MRADI WA UFUGAJI SAMAKI

No comments: