Wednesday, March 21, 2012

ZAWADI

Zawadi ni nini?
Ni kitu anachopewa mtu bila kutarajia au akiwa na matarajio kutokana na ama mazoea ya kupokea au mazingira yaliyotengenezwa kuchochea upatikanaji wa zawadi. Kwakuwa lengo ni kumfurahisha mlengwa yapo mategemeo ya kupokea upendo, huruma au faraja.

Zawadi zipo za aina nyingi sana,kuna pesa, mikufu, heleni,nguo,viatu n.k.

Mambo gani muhimu ya kujiuliza


Zawadi ni nzuri hakika lakini unapopewa na kabla hujaipokea ni muhimu ujiulize maswali yafuatayo:

Aliyenipa zawadi hii amefanya hivyo kutokana na mimi kumuomba, kumshurutisha au kuonyesha kuwa naitegemea?
 Wananchi au wadau wengine watakapojua nimepokea zawadi hii watanielewaje?
 Aliyenipa zawadi akirudi tena kwangu akiwa na jamaa au rafiki yake je! nitakuwa huru nisijisikie kuwa nina deni kwake au kuwa na mategemeo ya zawadi nyingine?
 Duru ya uwazi nitaiweza bila shida yeyote kwa kutangaza kwa wadau wengine bila wasi wasi wowote kuwa nimepokea zawadi?
Iwapo ikijulikana nimepokea zawadi wenzangu wataliona ni jambo zuri, la kawaida na la kuridhisha?


Maswali yote hayo juu yanategemea umepokea ZAWADI ya aina gani


ANGALIZO : Tuwe makini na zawadi tupewazo, zingine ni za moto, baridi na vugu vugu. Tumia upeo wako na akili yako kuchanganua, je anayenipa zawadi hii ana nia nzuri na mimi? Je! Zawadi hii ina maana gani kwangu? Nina ukaribu gani naye hadi anipe?Ukijiuliza maswali hayo waweza amua ufanyaje. Kila la heri katika upokeaji ZAWADI uendeleao kila mara.

NAWAPENDA WADAU WANGU, NAWATAKIA UJENZI MWEMA WA TAIFA/MATAIFA KWA UJUMLA

No comments: