Monday, June 18, 2012

LA FAMILLE GET TOGETHER DINNER @ NYUMBANI " NYEUPE NYEUPE ILITAWALA"

Kulikuwa na rahaajeee
Cute Smile na Leon Lee walijishindia Dollar 100
Baada ya kupita kwenye votes za watu kutaka wapige mabusu hadharani. Wakafunika
Wakaomba wachenjiwe wagawane hapo hapo kila mtu aendelee kuzitumbua usiku huo kwa raha zao
 Chezeaaaaa
 Da Joy ali pop in kusema Hellow

Washindi waliopendeza zaidi kutokana na kura za wana Famille no. 1 alikuwa ni Wise Monica Kaaya na no.2 alikuwa ni Ester Ulaya....walipata vijizawadi vidogo tu

Ila Party ijayo tutajitahidi pawepo na sponsors ili kuleta changamoto na kutoa Zawadi kubwa zaidi
Mwanzo mgumu

Ila kwa hicho kidogo kilichokuwepo kilichokuwepo kilinogajee
Picha ya pamoja LA FAMMILE
Waliohudhuria ni 1.Happy Happy, 2. Wanty 3. Sis 
4. Anna 5. Faraji 6. Marcell 7. GK 8. Cute Smile 
9. Leon Lee 10. Maggie 11. Monica 12. Mama Siyabonga a.k.a Boss Kitumbo 13. Pretty Dacha 14. Ester Ulaya 
15. Maggie na 16. Jide
Tukawa na msanii mpya wa Bongo Flava akamwaga cheche mtamfahamu hivi kaibuni

Pretty Dacha (ki model chetu) tunamtafutia Agency kama kuna mtu huko anahitaji chuma hiki hapa mkijaribu


 Maggie (Bi harusi mtarajiwa) na Marcell

 Leon Lee & Monica

 Anna & Happy
 Wanty & Ester Ulaya
 Melissa, Sis na Cute Smile
 Mwenye Black na white ni GK



 Washindi wa 1 na 2, Ester na Monica


Busu la 2012
Jumamosi ya tar 30 tukijaaliwa uhai
Tunakwenda kutembelea kituo cha watoto yatima walioandika barua kuomba msaada kwa LADY JAYDEE na friends

Kwa yoyote ambae hakuhudhuria La Famille Dinner
Na angependa kushiriki kutoa msaada tuwasiliane
e-mail: judyjaydee@yahoo.com

KUTOA NI MOYO

Tutaongozana na Bus la pamoja na mizigo yote itakabidhiwa kwa wahusika na haipitii mikononi mwangu

Asanteni kwa ushirikiano

WITH LOVE
JIDE

STORY NZIMA NA PICHA SHUKRANI LADY JAYDEE BLOG

Sunday, June 17, 2012

JUMAMOSI ILIKUWA NI SIKU FUPI SANA KWANGU

 Huku ni kwa-Tumbo Bagamoyo, nikwaonaga akina mama kama hivi natamani kila muda niwaamkie, heshima juu yao ni kubwa mnooooooooo
 Huyu mtoto alinisababisha niumie sana baada ya kuona hili kovu bado halijapona vizuri, wanasema mama yake alikuwa anachoma mabiwi shambani, akasikia mtoto analia kumbe kaangukia humo anaungua
 Na hapa bado hakijapona vizuri, ni mdogo hata bado hajajua kuongea vizuri, tuwe makini na watoto hasa kuwakinga na vihatarishi kama moto, maji,michanga n.k.
 Sasa kama hapa mtoto yupo jikoni, kidonda hakijapona na dada yake anachochea moto hajafunikwa hata nguo, nilimshauri mama mtu ajitahidi mtoto awe mbali kabisa na maeneo ya moto ili apone mapema....si mnajua kidonda cha moto kikipata joto la moto kinapata maumivu makali
Baada ya kazi iliyonipeleka wenyeji walinipa zawadi ya mahindi mabichi, ndani ya bag nyuma kuna machungwa na papai.

Kittens Follow The Leader

Friday, June 15, 2012

NGWE YA KWANZA IJUMAA YANGU INAISHA HIVI

 Nikiwa na Surveyor mwenzangu Site Mbagala
 Kazi ni kazi
 Fanya kazi mama, miaka yoooote uliyosoma ndo kazi uipendayo sasa unaifanya.....Shukrani kwa Mungu, I love my Job
 Tulikuwa na Mafundi wa Tanesco Site
 Tukifanya kazi ya kupanda Beacons
 Kuna mama alikuwa anakaanga dagaa na samaki
 Hapo anaelezea bei kila fungu
 Nikajitwalia dagaa wa kutafuna waliotoka motoni wa motooooo, kwa shilingi 500/-
Mlinzi aliyekuwa anatulinda na kutuonyesha Baadhi ya mipaka ya eneo kule juu ndo makazi yake

MNAKUMBUKA MAMBO YA WIMBOMBO NA ULINDI?????????

 Unapekechaaaaaaaaaa
Hadi moto unawaka....tulisoma kwenye history miti iliyokuwa inatumika kuwasha moto kwa asili kabla vibiriti havijaanza

TUANZE SIKU YETU HIVI