Wednesday, February 27, 2013

KUMBUKUMBU YA VITA YA MAJI MAJI SONGEA

Mashujaa wa vita ya Majimaji kabla ya kunyongwa

Wazee wetu wa kingoni wakiwa wamevaa kijadi na kucheza ngoma asili
Mgeni rasmi Balozi Kagasheki akiambatana na Chief Zulu kwenye maandamano
Mnara wa ukumbusho..... hapa ndo waliwanyonga mashujaa wa vita vya Majimaji Songea - Tanzania
Gwaride la heshima ukumbusho wa vita vya Majimaji 
Mama amepata mshtuko mkubwa baada ya milipuko ya heshima kumbukumbu ya vita ya Majimaji
Kaburi la Chief Songea Mbano
Chief Songea Mbano .. nduna wa nduna .. Jemedari wa wangoni .. shujaa wa vita ya Majimaji
Check number 61 out of 66 Majimaji war heroes .. Mkomanile ni mwanamke na nduna yaani sub chief.
Kikosi cha wapiganaji wa vita ya Majimaji wakiwa chini ya ulinzi ndani ya ngome ya Wajerumani
Area that Majimaji war extended.. tusiwabeze watu wa kusini hata siku moja ni mashujaa kweli hawakukubali kutawaliwa!
Maria With Davis Tillya chief cameraman Compass Communications and great grandson of Chief Songea Mbano hero

Picha kwa hisani ya Maria Sarungi

Tuesday, February 26, 2013

TUKUMBUSHANE: EPUKA KUFANYA MAMBO YAFUATAYO BARABARANI.

1. USICHEZE BARABARANI, KUSIMAMA, KUZUBAA, KUZURURA AU KUTANGATANGA BARABARANI.



2. USIWAACHE WATOTO WADOGO WATEMBEE PEKE YAO BARABARANI.


3. USIWEKE VIZUIZI HOVYO BARABARANI PASIPO KUTOA TAHADHARI, USIWAZUIE WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA KWA KUSIMAMA KATIKATI YA BARABARA YA WAENDA KWA MIGUU KWASABABU YOYOTE ILE.


4. USIFANYE MAANDAMANO AMBAYO HAYAONGOZWI NA ASKARI WA USALAMA BARABARANI AU HAYAZINGATII KANUNI NA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI.


5. USITUPE TAKATAKA HOVYO BARABARANI HASA VITU VYENYE NCHA KALI NA VITU VINAVYOWEZA KUSABABISHA UTELEZI NA HIVYO KULETA MADHARA KWA VYOMBO NA WATUMIAJI WA BARABARA.


6. USIMWAGE AINA YOYOTE YA MAFUTA BARABARANI, NI HATARI HUSABABISHA UTELEZI NA KUHARIBU BARABARA.


7. USIHARIBU ALAMA ZA BARABARANI.


8. USITEMBEE USIKU BILA TAA AU BILA KUVAA NGUO ZINAZONG'ARA ILI UWEZE KUONEKANA KWA URAHISI KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA HUSUSANI MADEREVA

Friday, February 22, 2013

WATOTO NI BARAKA NDANI YA NYUMBA.....HAIJALISHI UMEZALIWA KATIKA FAMILIA IPI

Wiz Khalifa na mwanaye

Nawatakia Ijumaa njema, tuzidi kuwafariji watoto wetu hasa waliomaliza Form IV mwaka huu, tutafute kila namna ya kuongea nao wasiendelee kujinyonga hasa wale waliofanya vibaya, hii inasikitisha mno.

Thursday, February 21, 2013

KILA KAZI NA CHANGAMOTO ZAKE: WAREMBO WAKIWA STEJINI WAKIWAKILISHA MAVAZI









MAWAKALA WA PESA KUPITIA MITANDAO YA SIMU KUWENI MAKINI

Huyu Tapeli tulimshuhudia live akila kichapo

 Tapeli aliyefahamika kwa jina la Rashidi Hussein (27), Mkazi wa Shule ya Msingi Kigogo 'C' leo jioni amepokea kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali baada ya kukamatwa akitaka kumtapeli kiasi cha tsh. 500,000/- kutoka kwa mama mmoja ambaye anaendesha biashara yake ya M-Pesa eneo Kijitonyama Sokoni jijini Dar es Salaam.
Akisimulia mkasa huo mama huyo ambaye hakupenda jina lake litajwe, alisema kuwa majira ya saa 11 kasoro jioni walifika vijana wapatao watatu ambao walikuja kwa nia ya kuwekewa pesa kiasi cha tsh. 5,000/- ndipo mama huyo alipompa simu ili aandike namba yake tapeli Rashidi Hussein, aliandika namba na kumbeep mwenzake kwa siri ili apate namba ya mama huyo na yeye alihihifadhi kwa siri namba ya rafiki yake kwenye simu ya mama huyo kwa jina la M-Pesa.
Mama huyo alioona tapeli Rashidi anachukua muda mrefu kuandika namba yake kwenye simu ndipo alipoamua kumnyang'anya simu ile na kukuta amehifadhi namba yake kwa jina la M-Pesa. Alipoona kuwa tapeli Rashidi amehifadhi namba yake alichukua jukumu la kuiandika namba ile kwenye karatasi na kuifuta kwenye simu yake na hapo ndipo akishtuka kuwa kuna mchezo anataka kuchezewa.
Aongeza kuwa baada ya kuwa amemaliza kumhudumia tapeli Rashidi kwa kumuwekea tsh. 5,000/- katika simu yake. Tapeli Rashidi aliondoka lakini baada ya muda mfupi alirejea na kumuuliza mama huyo kuwa amerudi kutoa pesa kwenye M-Pesa kiasi cha tsh. 500,000/-, alimjibu sawa na hapo ndipo alipompigia simu aliyedai ni Mjomba wake kwa kumwambia tuma basi hiyo hela.
Mama huyo anasema, wenzake ambaye mara ya kwanza aliwabeep namba ya yake alituma mesaji ya uongo kwa mama yule na kuonyesha namba ya kawaida kuwa imetoa kiasi cha tsh. 500,000/- na hapo ndipo alipowaita vijana waliokuwa maeneo ya kibanda hicho na kuomba msaada na kufanikiwa kumkamata tapeli Rashidi na kuanza kumpa kichapo ili awaseme wenzake. Wenzake ambao walikuwa wakimsubiria pembeni baada ya kuona hayo alikimbia.
Mama huyo alishukuru kufuta namba ile maana bila ya kufuta mesaji ingeingia kwa jina la M-Pesa na kujikuta ametoa hela kiasi hicho cha tsh. 500,000/= na kumpatia tapeli Rashidi. Alitoa shukrani kwa majirani zake ambao walionyesha ushirikiano katika kumkamata tapeli huyo ambaye alikutwa na sim card za mitandao mingine pamoja na kitambulisho cha kupiga kura.
Pichani ni wananchi wakitoa kipigo kwa tapeli Rashidi.
 Wananchi wakimwadabisha tapeli Rashidi Hussein (27), Mkazi wa Shule ya Msingi Kigogo 'C'(ambaye hajavaa shati.
 Tapeli Rashidi Hussein (27), Mkazi wa Shule ya Msingi Kigogo 'C'akijitetea mbele ya wananchi wenye hasira kali.
 Kila mmoja akiwa na hamu ya kutoa kichapo kwa tapeli Rashidi Hussein ambaye alikamatwa na mama mwenye kibanda cha M-Pesa.
Tapeli Rashidi Hussein (27), Mkazi wa Shule ya Msingi Kigogo 'C' akilia huku pembeni yake kukiwa na sim card nyingi ambazo alikuwa akitumia kufanya utapeli huo.
 Wananchi wenye hasira kali wakitoa kichapo kwa tapeli Rashidi Hussein.
 Tapeli Rashidi Hussein (27), akimwagika damu baada ya kichapo hicho.
 Wananchi wakishauliana kumpeleka polisi baada ya kumpa kichapo, huku wengine wakikataa na kusema haina haja ni bora wamuue jambo lililopigwa na wengine.
Akivushwa barabarani kupelekwa kituo cha polisi mabatini jijini Dar.
 Baada ya kuvushwa barabara tapeli huyu alitaka kukimbia ndipo alipopigiwa mayowe ya mwizi na kumfanya asimame.
 Msafara wa kwenda polisi.
 Mama mwenye kibanda cha M-Pesa (aliyejishika kiuno) alinusurika kutapeliwa baada ya kumshitukia tapeli huyo.

 Mama akiwa katika hali ya mshangao baada ya kunusurika kutapeliwa kiasi cha tsh. 500,000/-
 Hiki ndicho kitambulisho cha tapeli huyo mara baada ya kusachiwa na kukutwa na sim card nyingi za mitandao tofauti tofauti.

SOURCE: www.kajunason.blogspot.com

HEALTHY: SPECIAL FRIED RICE



Ingredients

SPECIAL FRIED RICE
Enough for 2 rice. cooked 10 minutes and drained
2 eggs. beaten
a handful Peas
a handful sweetcorn
8 large or 12 small prawns (cooked)
1 tablespoon stir fry oil or sesame oil
2 tablespoons soya sauce
1 table spoon Sweet Chilli Sauce
2 large slices thick cut ham

Method

Heat up the oil in a deep frying pan.

Add the egg and using a spatula or wooden spoon start to move it about as if making scrambled egg. Make sure you keep seperating it so it doesnt become a big lump.

Once its cooked add the rice and mix with the egg.

Add the peas and sweetcorn, ham and prawns and heat through. Then add a splash of soya sauce and a splash of sweet chilli sauce.

Serve warm with a stirfry or chinese curry.


Tips

Some people may wish to add salt. I leave that out as I dont like it but many people are used to having very salty food.

A good tip for this recipe which I've done many times before is to not over stir the rice as it becomes stodgy and ends up being very gooey!

By 

Tuesday, February 19, 2013

HIZI NI BAADHI YA SHULE ZILIZONISIKITISHA MNO, WALIMU NA WAZAZI WANA HALI GANI?

S2574 MIBUYUNI SECONDARY SCHOOL

S4274 NDAME SECONDARY SCHOOL

S3732 CHITEKETE SECONDARY SCHOOL

S4355 MAENDELEO SECONDARY SCHOOL

S2833 KWAMNDOLWA SECONDARY SCHOOL

S4750 KIKALE SECONDARY SCHOOL

S3454 TONGONI SECONDARY SCHOOL

S1930 J. M. KIKWETE SECONDARY SCHOOL

S4914 MEMBE SECONDARY SCHOOL

S4915 DR JOHN SAMWEL MALECELA SECONDARY SCHOOL

S4416 MIZENGO PINDA SECONDARY SCHOOOL

S4509 DR. WILBROAD SLAA SECONDARY SCHOOL

S0697 KIGWE SECONDARY SCHOOL

S2306 BUSANDA SECONDARY SCHOOL

S4381 KILELENI SECONDARY SCHOOL

S4441 LAKITATU SECONDARY SCHOOL

S4256 CHOKOCHO SECONDARY SCHOOL




HIZI NI BAADHI TU, INAUMA SANA KUONA VIJANA WENGI WAMEFELI HIVI, HATIMA YAO NI NINI?


GONGA HAPA UONE MATOKEO HAYO

MVUA INAYOENDELEA KUNYESHA LUSAKA - ZAMBIA

 Mvua ni baraka....ikizidi mambo huwa hivi
 Madimbwi yakutosha

 Baadhi ya Bara bara zimejaa maji kwelikweli
Asante sana Patience kwa picha hizi