Wednesday, October 10, 2012

CHUMBA CHA FIRST CLASS CHA TRAIN YA RELI YA KATI KIPO HIVI: MAMLAKA HUSIKA LIANGALIENI HILI KWA JICHO LA PILI

Vitanda vimeisha kweli kweli, inakuwa haina hadhi tena kuita First Class, marekebisho yafanywe


 Hii niliambiwa ni AC
 Kwa sasa zipo kama mapambo...hazifanyi kazi
 Sinki la maji, abiria huweka mizigo yaoo kama uonavyo
Testing kama maji yanatoka.........maji yapo muda wote kwa hili mmweweza, issue nyingine ni panya na mende, wengi mnoooo

Sunday, October 7, 2012

ILISHEREHEKEWA NAMNA AMBAYO SIKUWAHI KUWAZA: TAREHE 04/10/2012

Hii iliandaliwa na Husband, niliona picha tu FB nikawa najiuliza mbona sioni kitu Live.........jioni tulikuwa na shughuli ya kwenda kupokea Wakwe Ubungo.....tukawapeleka Mbezi walikotakiwa kufikia.....si ndo nikashangaa Cake inaletwa pale.....nilifurahi sana ikakatwa na wazazi na ndugu kibao tukashangilia ikawa kifamilia zaidi
 Mida ya saa 5 usiku tukarudi home tukapita kwanza Friends Pub.........ndo nikakuta Cake nyingine kutoka kwa mdogo wangu Faraji.......bonge la mshangao
 Nikaambiwa niikate tuile pale pale, shughuli ikaanza
 Shangwe hasa, kila aliyekuwa analishwa alikuwa anaimbwa jina lake likireflect uhusiano nilionao naye........ilikuwa raha sana
 Babu babu babu.................
 Rafiki rafiki rafiki...............
 Kata cake tuleeeeeeeeeeeeeeee
 Nikaanza na babu....
 Classmate classmate......anaitwa Nisile
 Jirani jirani jiraniiii................................
hahahhahahha Huyu wakamwita Manji manji manji............maana jana yake ndo ilikuwa timu ya Yanga na Simba....sasa alikuwa anauendesha mjadala huo balaaa ingawa ni Simba na mimi ni Yanga akasema unamlisha Manji hahahahahhaha
 Ikawa zamu ya Caunter caunter caunter.......................
 Mteja mteja mteja............................
 hahahhahahaha hapa wakaimba Baba Baba Baba.............
 Siku hiyo ilikuwa ni kucheka tu.......hadi matukio mengine mpiga picha alikuwa anayasahau 
Namalizana na maswala ya Cake nikakabidhiwa box lina zawadi hizi, fahari ya Tanzania Shukrani sana Monica Kaaya kwa zawadi hizi

ASANTENI SANA WAPENDWA WANGU MLIONISAIDIA KUFURAHIA HII SIKU ILIKUWA NJEMA MNO......KUANZIA WAZAZI, HUBBY  HADI MARAFIKI WOTE
AMEN

Friday, October 5, 2012

TUCHEKE LEO NA VITUKO VYA TOM NA JERRY

MBINU ZA KUACHA UVUTAJI WA SIGARA aka FEGI!!!!


Miongoni mwa mambo magumu kabisa katika ufanikishaji wake ni mtu kuachana na uvutaji wa sigara. Watu wengi wamekuwa wakionywa kuachana na uvutaji wa sigara kwa sababu ya madhara yake, lakini wamekuwa wakishindwa kutokana na kukolewa na kiwango cha Nikotini inayopatikana katika tumbaku. 

Vijana wengi wamekuwa wakijiingiza katika uvutaji kwa kuf
uata mkumbo, lakini baadaye wanapokuja kutambua kuwa wako katika hatari ya kuambukizwa au pengine wana ugonjwa wa kifua kikuu, wanakuwa katika wakati mgumu wa kuachana na uvutaji huo. Wengi wao wamekufa huku makundi kwa makundi wakitangatanga kutafuta suluhu ya kuchana na uvutaji, si tu kwa sababu ya kuhofia ugonjwa, bali hata kukosa uwezo wa kununua bidhaa hiyo.

LOVE SIGN





Thursday, October 4, 2012

HAPPY BIRTHDAY TO ME

Shukrani sana kwanza kwa Mungu kunijalia uhai hadi leo, Shukrani kwa wazazi wangu walio bega kw bega nami hadi leo, shukrani kwa Mume wangu Mpendwa ambaye yuko sambamba nami hadi leo na ananijali kwa lolote litokealo upande wangu, niwashukuru Marafiki wangu woteeeee waliopo nami siku zote, pia asanteni wooooote mnaoendelea kunitakia heri katika siku yangu hii ya kumbu kumbu ya kuzaliwa, Namuomba Mwenyezi Mungu asiniache kamwe, bali aendelee kuwa nami daima na kuwea kutimiza ndoto zangu Amen

Monday, October 1, 2012

MNADA WA IPULI-TABORA WAZIDI KUPAMBA MOTO

 Kila Jumamosi huwa ni mnada wa wanyama....na kuchoma nyama na vinywaji, hautofautiani sana na ule wa Dodoma
 Na hii ilikuwa ni siku ya Jumamosi tarehe 29/09/2012
 Mifugo ikitawaliwa kwa namna hii
 Bidhaa mbali mbali zikiuzwa


 Yebo yebo kwa wingi
 Mazizi ya Wanyama empty baada ya kuuzwa 
 Zana/silaha za kujilinda

 Upinde na Mishale sokoni
 Testing




 Tax, Boda boda na baiskeli zilikuwepo kutoa usafiri wa fasta kwa warudio


 Mifugo ambayo haikupata soko iliswagwa kurudi home