Sunday, October 7, 2012

ILISHEREHEKEWA NAMNA AMBAYO SIKUWAHI KUWAZA: TAREHE 04/10/2012

Hii iliandaliwa na Husband, niliona picha tu FB nikawa najiuliza mbona sioni kitu Live.........jioni tulikuwa na shughuli ya kwenda kupokea Wakwe Ubungo.....tukawapeleka Mbezi walikotakiwa kufikia.....si ndo nikashangaa Cake inaletwa pale.....nilifurahi sana ikakatwa na wazazi na ndugu kibao tukashangilia ikawa kifamilia zaidi
 Mida ya saa 5 usiku tukarudi home tukapita kwanza Friends Pub.........ndo nikakuta Cake nyingine kutoka kwa mdogo wangu Faraji.......bonge la mshangao
 Nikaambiwa niikate tuile pale pale, shughuli ikaanza
 Shangwe hasa, kila aliyekuwa analishwa alikuwa anaimbwa jina lake likireflect uhusiano nilionao naye........ilikuwa raha sana
 Babu babu babu.................
 Rafiki rafiki rafiki...............
 Kata cake tuleeeeeeeeeeeeeeee
 Nikaanza na babu....
 Classmate classmate......anaitwa Nisile
 Jirani jirani jiraniiii................................
hahahhahahha Huyu wakamwita Manji manji manji............maana jana yake ndo ilikuwa timu ya Yanga na Simba....sasa alikuwa anauendesha mjadala huo balaaa ingawa ni Simba na mimi ni Yanga akasema unamlisha Manji hahahahahhaha
 Ikawa zamu ya Caunter caunter caunter.......................
 Mteja mteja mteja............................
 hahahhahahaha hapa wakaimba Baba Baba Baba.............
 Siku hiyo ilikuwa ni kucheka tu.......hadi matukio mengine mpiga picha alikuwa anayasahau 
Namalizana na maswala ya Cake nikakabidhiwa box lina zawadi hizi, fahari ya Tanzania Shukrani sana Monica Kaaya kwa zawadi hizi

ASANTENI SANA WAPENDWA WANGU MLIONISAIDIA KUFURAHIA HII SIKU ILIKUWA NJEMA MNO......KUANZIA WAZAZI, HUBBY  HADI MARAFIKI WOTE
AMEN

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Aise! kweli inaonekana ulikuwa na wakati mzuri sana ni safi kuwa na marafiki na pia kufaana wakati wa shida na pia raha. Endeleza hilo..nimetamani zaidi hizo zawadi za vitenge:-)