1. Ushkaji Feki sio Deal kwangu bora uwe adui kuliko kuwa snitch.
2. Sipendi sana kugombana na watu isipokuwa tu pale inapobidi.
3. Sio mjuaji sana japo najua mengi kwenye maisha kupitia niliyoyaona na yaliyonifika.
4. Usipende kuwa karibu na mimi kwa kuwa nina kitu flan au kuna kitu unafaidika ili kutimiza malengo yako maana ipo siku hivyo vitu havitokuwepo ama usipate nafasi ya kuvifikia.
5. Ukimpa deal mshkaji mwingine wakati hata mimi inaweza nifaa kama huyo uliempa na baadae uka act kama mimi ni mshkaji wako zaidi ni usaliti wa wazi
6. Usipende sana kujua vitu vyangu na kuficha vya kwako.
7. Ishi maisha yako usitambalie kivuli changu kufanikisha mipango yako kwa gear ya urafiki ama kunipa support kumbe si kweli.
8. Ushkaji wa kutojitolea ni uongo mtupu.
9. Chako chako na changu chako hapana hiyo kwangu.
10. Ishi kwa upendo usitegemee cha ndugu.
Peace & Love Africa !!!!!
2 comments:
oh! ni furaha ilioje ya kwamba upo hewani tena karibu sana.. nimeipenda hiyo namba kum....i Ishi kwa upendo usitegemee cha ndugu!
Asante sana dada....ila bado sijarudi vizuri...nachungulia tu
Post a Comment