Friday, December 21, 2012

Waombaji wote waliochaguliwa kwenda Msumbiji kusoma 2012/2013 kwa utaratibu wa TAMOSE

TANZANIA - MOZAMBIQUE STUDENTS EXCHANGE PROGRAM   (TAMOSE)

Waombaji wote waliochaguliwa kwenda Msumbiji kusoma 2012/2013 kwa utaratibu wa TAMOSE, wanatakiwa kufika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi tarehe 31/12/2012 kwa ajili ya kupewa maelekezo husika. Wanatakiwa kujiandaa na kuwa tayari kwa safari kwenda Msumbiji Jumatatu tarehe 2/01/2013 au Jumatano 6/01/2013. 

Mkutano wa maelekezo utaanza saa 3:00 asubuhi katika Ukumbi wa mikutano hapa Wizarani. Itabidi kila mmoja ajigharimie kuja Dar Es Salaam na kwa muda wa kusubiri safari. Kila mwombaji atakayeona taarifa hizi amwarifu mwenzake.
 

Kajigili, A.J.
Mratibu wa TAMOSE
Idara ya Elimu ya Juu
Kwa maelezo zaidi: 0713 401623.

No comments: