Friday, September 7, 2012

MAREHEMU KANUMBA BADO ANAJADILIWA

PASTOR EMMANUEL MYAMBA AFUNGKA NA KUDAI KANUMBA ALIMTONYA KUHUSU FREEMANSON...!!!

Na Jelard Lucas - Global Publishers
MSANII ‘first class’ katika kiwanda cha filamu za Kibongo, Emmanuel Myamba ameibuka na kudai kuwa marehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake aliwahi kumtonya kuhusiana na masuala ya Freemanson.

Akifunguka kuhusu issue hiyo hivi karibuni, Pastor Myamba alisema siku hiyo Kanumba alitumia muda wake mwingi kuzungumzia masuala ya Freemanson, jambo ambalo lilimfanya abaki na maswali mengi kichwani.

“Nakumbuka sana Kanumba aliwahi kuzungumzia sana masuala ya Freemanson, alikuwa ananionyesha kwenye intaneti jinsi Freemanson wanavyofanya kazi zao lakini sikufahamu kama alikuwa na mkakati wa kujiunga nao au vipi,” alisema Myamba ambaye hivi karibuni alizindua chuo chake cha masuala ya filamu chini ya Kampuni yake ya Bornagain Film Productions.

Kanumba na Pastor Myamba walikuwa marafiki wa karibu sana na baada ya Kanumba kufariki, taarifa za kwamba alikuwa Freemasons zilizagaa sana kiasi cha kuwashangaza wengi.

No comments: