Tuesday, August 7, 2012

JANA JIONI 6/8/2012........NDO HALI HALISI YA JIJI LETU

Kituo cha Dala dala ndo kama hivi, abiria wakisubiria usafiri
Dala dala ilipofika wapo waliotumia technique ya kupitisha kabisa mizigo dirishani ikiwa ni guarantee ya kupata siti
Mvumilivu hula mbivu...wapo walioendelea kusubiri wakiamini daladala wapandazo zitafika waondoke
Kasheshe huwa ni kwa Wanafunzi zaidi, ona wanavyojitahidi walau wapate upenyo wapande na abiria nao wamekaba kweli kweli........lazima kieleweke tu
Duh.......hapo sasa kama kuna vibaka wapo walioibiwa


Kuna mdada ilibidi aombe apite upande wa Dereva...yote hii ili apate siti au aweze ingia ndani ya basi maana mlangoni kupenya ni shughuli
Nani alisema siku hizi dala dala za mbagala hawaingilii dirishani???? check wakaka hao walivyobusy lol
Madereva wa dala dala huwa wana akili wazijuazo....ona hiyo kubwa ilivyotokezea upande ambao sio wake akasababisha mfungamano wa magari......maskini huyo Learner sijui alitetemekaje baada ya kuona hiyo hali.

NAWATAKIA KAZI NJEMA WAPENDWA WANGU WOTE......MIMI PENDA SANA NYIE

4 comments:

R.Ngaiza said...

Usafiri wa dar si mchezo hasa mbagala lol nilishuhudia mtu akipigwa mangumi ya kichwa akijaribu kupitia dirishani. Watengeneze hayo ma train tena wangeelekeza pande za mbagala make kunahitaji msaada zaidi.

Ester Ulaya said...

Yaani my wii hizo train zikija nitafurahi sana, zitatusaidia mnoo

Yasinta Ngonyani said...

Hakika taabu sana kuangalia tu inatosha....wafanye haraka na hizo treni jamani usafiri huo duh kichwa kinauma...

Ester Ulaya said...

Maana ile gombania gari ukifika home mwili unauma kama ulikuwa unapigana