Thursday, July 26, 2012

KUMEKUCHA TAMASHA LA “CHAGGA DAY CULTURAL FESTIVAL 2012”


  Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya MyWay Entertainment, Paul Maganga (Kulia) akielezea juu ya tamasha maalum la siku ya Wachaga  lililodhaminiwa na Pepsi, litakalofanyika siku ya Jumamosi Julai 28,Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, ambapo pia litasindikizwa na bendi za Msondo Ngoma, Twanga Pepeta na vikundi vingine vya ngoma ya asili, (Kushoto) Ni Fredrick Mtaki, Afisamahusiano wa kampuni hiyo
BENDI  zenye ushindani mkubwa nchi za Twanga Pepeta na Msondo Ngoma zinatarajiwa kupiga shoo ya aina yake kwenye tamasha la siku ya Wachaga, (Chagga Day 2012), Julai 28, viwanja vya Leaders.
 
Akizungumza na waandishi wa habari  mapema leo ukumbi wa Udara habari Maelezo, ijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya MyWay Entertainment, Paul  Maganga walioandaa tamasha hilo lililoadhaminiwa na kampuni ya SBC Tanzania Limited,kupitia kinywaji cha Pepsi, alisema  siku hiyo itakua ya aina yake kwa watu mbalimbali na familia zao watakaojitokeza kufurahia kwa pamoja tamaduni za kabila hilo la Wachaga sambamba na makabila mengine yatakayoshiriki tamasha hilo.
 
“Siku hiyo ni ya pekee, kwa familia kujifunza mambo ya utamaduni  wa kabila hilo la Chaga, na makabila mengine  na burudani kutoka kwa bendi hizo za Twanga na Msondo,  pamoja na vikundi vingine vya ngoma ya asili ” alisema  Maganga
 
Pia alisema kua, kutakua na wazee wa  mila ambo watazungumzia asili la kabila la wachaga huku vyakula na vinywaji vya asili kutoka mkoa wa Kilimanjaro, Kiburu, ndafu, shiro, kitawa, macharari, ngararimo, ng’ande, kisusio, mtori, Kisusio na vingine vingi vitakuwepo siku hiyo.
Aidha, Siboka alisema  baada ya Tamasha la hilo la ‘Chaga day’, litafuatia tamasha lingine litakalofanyika Mkoa wa Kilimanjaro, Desemba 22 ambalo litapambwa na sherehe mbalimbali
 
Aidha, Maganga alisema kua, wataendelea kufanya matamasha haya kwa karibu makabila yote yaliyopo hapa nchini ilikuwezesha jamii kutambua mila zao  sambamba na kudumisha utamaduni wa Mtanzania kwa  kuwakumbusha tamaduni zao hii pia itakua ikijenga na kudumisha mahusiano baina ya  makabila mbalimbali  nchini Tanzania.
 
Pia anasema kua, watazania watakao hudhuria tamasha hilo, watapata kujua chimbuko la kuweko kwa  tamaduni zao  yaani mashujaa wa makabila yao, viongozi na machifu waliotawala jamii zao.

5 comments:

ray njau said...

UNAPOTAJA JINA KILIMANJARO KWA HAKIKA UNATAJA TANZANIA KUTOKANA NA UMAARUFU WA MLIMA KILIMANJARO AMBAO NI MAARUFU KULIKO YOTE AFRIKA.NGOMA KUBWA YA ASILI YA WACHAGGA NI IRINGI. IRINGI HUCHEZWA KATIKA MDUARA HUKU WATU WAKIWA WAMESHIKANA MIKONO IKIWA NI ALAMA YA UPENDO NA MSHIKAMANO WA KIFAMILIA .ZAO KUU LA BIASHARA NA UCHUMI KWA WACHAGGA NI KAHAWA CHINI YA CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA [KNCU].WACHAGGA WANAISHI KWENYE WILAYA NNE ZA MKOA WA KILIMANJARO AMBAZO NI SIHA;HAI;MOSHI NA ROMBO KWA MPANGILIO UFUATAO:

---------------------------------------------------------------------------------------------------------

1.WASIHA

2.WAMACHAME [ WILAYA YA SIHA NA HAI]

3.WAMASAMA

--------------------------------------------------------------------------------------------------------

4.WAKINDI

5.WAKIBOSHO

6.WAURU

7.WAOLDMOSHI

8.WAMBOKOMU [ WILAYA YA MOSHI ]

9.WAKIRUA

10.WAKILEMA

11.WAMARANGU

12.WAMAMBA

13.WAMWIKA

---------------------------------------------------------------------------------------------------------

14.WAKENI

15.WAMKUU

16.WAMASHATI [ WILAYA YA ROMBO ]

17.WASSERI

18.WANGASA

---------------------------------------------------------------------------------------------------------WAKAMBA WALIUITA MLIMA HUU "KIMA JA JEU[MLIMA MWEUPE];WAMASAI WALIUITA"OL DONYO EIBOR"[MLIMA MWEUPE];WATAITA WALIUITA NJARO[KILIMA CHA MUNGU];WACHAGGA WALIUITA KIPOO[KIBO] AU KILIMA CHA NJARO [KILIMA CHA MUNGU]

------------------------------------------------------------------------------------------------------

"WELCOME TO TANZANIA THE LAND OF KILIMANJARO,ZANZIBAR,THE SERENGETI AND THE BUSINESS BRIDGE TO GREAT LAKES COUNTRIES VIA DAR ES SALAAM PORT"

---------------------------------------------------------------------------------------------------------

Ester Ulaya said...

Kaka Ray umetisha, yaani unawafahamu kweli...au akina Njau ni wa huko?

ray njau said...

@Ester wa Ulaya;
Hakika jasiri haachi asili na muacha asili ni hasidi na hana akili.Kwetu ni huko Mkolowony,Mamba Kusini_Moshi Vijijini.Mimi ni asilia lakini mdau na mtetezi wa lugha ya Kiswahili.

ray njau said...

"Mchagga asilia,mdau na mtetezi wa lugha ya Kiswahili"

ray njau said...

Hiyo ngoma ya iringi watani zetu wanatuambia kuwa zamani ilizechezwa bila kushikana mikono lakini kila ngoma ikiisha watu wanajikuta watupu mifukoni mwao.Kutokana na utata huo azimio la uchaggani likapitisha amri ya kucheza kwa kushikana mikono ili kila abiria aweze kuchunga mizigo yake.Hapa ni kuwaza kiutani tu!!!