Monday, October 27, 2014

HOUSE GIRL AMCHOMA KISU MTOTO JICHONI NA KICHWANI : MUNGU TULINDE WANAO

Dada wa kazi (Housegirl), aliyetajwa kwa jina moja la Rachel, mkazi wa Tabata-Shule jijini Dar, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuchukua kisu jikoni kisha kumchomachoma nacho mtoto, Samwel John (4) anayeishi nyumba ya jirani.
Kwa upande wake House girl alipoulizwa ni kwa nini alifanya kitendo cha kinyama kiasi hicho alisema kuwa alikuwa akitamani kumtoa jicho mtoto huyo.
“Alisema kuna shetani au roho ilikuwa ikimtuma amng’oe macho mwanangu,” alisema baba wa mtoto huyo anayejulikana kwa jina la John.

source: EATV

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Ama kweli huu ni ukatili wa kinyama haswa...Mlio na wafanyakazi wa ndani muwe makimi.