Ikiwa leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mrembo Nancy Sumary, tujikumbushe mahojiano aliyowahi kuyafanya mwaka 2005 ambapo alifanya vizuri sana kwenye maswala ya urembo. Twende pamoja hapo chini kufuatilia mahojiano hayo
Lengo likiwa ni kuonyesha kuwa Nancy
Sumary alijiamini kwa kiasi gani na mwenye matumaini makubwa wakati
wa maandalizi yake kuelekea Miss World, na alipewa sapoti ya kiasi
gani na kamati ya Miss Tanzania ili angalau aweze kufanya vizuri
katika shindano hilo.
Baada ya mawasiliano ya hapa na
pale na mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga ndipo
nilipokutana na MissTanzania Nancy Sumari kwenye ofisi za kamati hiyo
zilizopo jengo la Mavuno House, ghorofa ya nne na kufanya mahojiano
naye kama ifuatavyo.
Mwandishi
: Miss
Tanzania Nancy Sumary hujambo dada?.
Nancy
: Mimi
sijambo kaka namshukuru Mungu.
Mwandishi
:
Tunaomba utupe historia yako kwa ufupi.
Nancy
: Anatoa
kicheko na kuonyesha tabasamu la kuvutia huku akianza kwa kusema
“Mimi nimezaliwa miaka 19 iliyopita na nimepata elimu
yangu nchini kenya, ambapo nilisoma huko mpaka kidato
cha nne katika shule inayoitwa Maasai High School.”
Mwandishi
:
Kama unavyojua unakabiliwa na kazi ngumu ya kuwatoa kimasomaso
Watanzania kwenye shindano la Miss World vipi maandalizi yako
yamefikia wapi hivi sasa.?
Nancy
: Kwa
ujumla maandalizi sio mabaya yanaendelea vizuri na ninapata msaada
mkubwa kutoka kamati ya Miss Tanzania nafikiri nitafanya vizuri tu.
Mwandishi
: Unaweza
kutupa ratiba yako ya kila siku jinsi unavyoipanga na kuifanyia kazi
katika kujiandaa.?