Friday, August 3, 2012

MTOTO KAOKOTWA......ANAYEMFAHAMU AJITOKEZE


Mtoto ameokotwa eneo la PPF Tower, Jijini Dar Es Salaam saa sita mchana wa leo. Amekutwa amelala chini eneo hilo.

Ameletwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Askari wa Central Police. Mtoto huyu anakadiriwa kuwa na umri wa mwaka mmoja na nusu hivi, kwa hiyo hawezi kuongea.

Yeyote anayemfahamu mtoto huyu au wazazi wa mtoto huyu ajitokeze na kutoa taarifa sahihi kwetu kupitia namba yangu 0755 64 86 3
6 au 0715 64 86 36.

Mtoto tunaye Hospitalini, anaendelea kuhudumiwa. Tafadhali sambaza barua pepe hii.

Imetolewa na;
Aminiel Buberwa Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi

Hospitali ya Taifa Muhimbili

1 comment:

ray njau said...

Habari ni zana muhimu maishani nasi tuifanyie kazi hiyo taarifa rasmi kutoka ofisi ya uhusiano MNH.@ester tunathamini sana kwa kutuunganisha na taarifa hii muhimu kijamii.Nakutakia afya njema,baraka tele,ufanisi bila nukta na kila jambo jema liandamane na nyayo zako njema sana.Salamu!!!