Monday, March 26, 2012

UCHAFU! UCHAFU! UCHAFU

Wakati Jiji linajitahidi kupingana na uchafu, watu wengine wanaona sifa kuhifadhi makorokoro ambayo hayatumiki na yameshapitwa na wakati majumbani kwao
Mpaka nimelileta hili, limenikera sana, na mtu ameshashauriwa sana atoe hataki kutoa yeye anaamini ipo siku yatatumika na kuwa siyo mauchafu tena
Hivi inakuwaje madude yameisha hivi halafu unakuta mtu kayahifadhi kila kona? nafuu hata angekuwa anayatumia kuyafanya madekio lakini yamening'inia tuuuuuuuu
Chumba kinaonekana kujaa makoro koro, nayaita makoro koro kwakuwa yaonekanavyo tu ni madude yaliyopo bila kazi, ni kuhifadhi panya tu hapa
Sasa madude kama haya ukiyatupa una hasara gani? walau hizo mbao tumia kama kuni ili usione ni hasara, tokea mwaka jana nayaonaga hapo hapo
Kila kona kuna madude, hivi jamani mtu kama huyu aelimishwaje????????
Vitu ambavyo hawezi kuvitumia tena , na kila mara wabeba uchafu wanapita, kwanini hawaruhusu wayabebe?
Hayo madude wanaanika na vitaulo juu yake, ni kwamba haoni tatizo makoro koro kuwa hapo
Tatizo ukimshauri ayatoe anajibu, mbona hayo mazima yatafanya kazi tu, ndugu mdau hebu nisaidie hapa yana uzima gani haya?
Mara nyingi tuna tabia ya kuhifadhi vitu na kupata uchungu kuvitupa, lakini angalia ni kitu gani cha kuhifadhi, vingine vyaweza kuwa madhara aisee
Ukweli upande wangu bado hainiingii akilini
Bonge la Nyumba, lakini kila mahari yamehifadhiwa haya madude, kama sehemu ya dampo
 Majani ya miwa yana zaidi ya miezi miwili hapa hapa

Hivi ndivyo baadhi ya watu wakiamini makoro koro husaidia baadae kumbe ni kero kwa jamii, nafuu hata kuwuzia wale wakusanyao scraper upate japo kitu, kwani kuhifadhi hivi muda mrefu kutu inazidi, panya na wadudu hatari ndo yanakuwa makazi yao, kuna usalama hapa kweli???????

ANGALIZO: Huku ni Kinondoni na uchafu wote huo upo ndani ya gate, yangekuwa nje labda city ingeshayatoa,nafuu ingekuwa garage, lengo si kumpublish muhusika, lengo ni kuwaeleza/kuwafikishia ujumbe na wengine wenye tabia hizi waache, muhusika kaelezwa sanaaa, ila mbishi mno, kwani bwana afya akizungukia maeneo haya ni shida, pia ni hatari kwa watu waishio hapa, tujirekebishe kwenye hili

8 comments:

Jana ★ said...

Very sad pics :(
Un besito y feliz lunes
http://janakitchen.blogspot.com

Ester Ulaya said...

sure Jana

Majoy said...

Yani sio huyo tu dia kuna wengi sana wenye tabia kama hizo wengine wanatunza machupa ya perfume au madumu ya mafuta jikoni basi kwa madai yatapata matumizi matokeo yake hugeuka uchafu na kuziba nafasi bila sababu za msingi.

Ester Ulaya said...

UMEONA EE mAJOYY, YAANI INAKERA, SIJUI KWA NINI HATUTAKI KUBADILIKA

Maggie said...

ahahahaaaaa khaa hapa mbona kama kwa annihiii ehehehehee kwa baba mwenye nyumba hapa. SIO SIRI MIMI HUWA NAKEREKAA NA NIMEGUNDUA WAZAZI WETU NDO VIONGOZI WA KUHIFADHI VITU WASIVYOTUMIA WANADAI ETI NI KUMBUKUMBU.

Ester Ulaya said...

hahahahaha Maggie kwa baba fudenge, yaani ukweli anaboa sana, wanahifadhi halafu hata hawatumii tena, nadhani wanasikitikia hela zao labda walizonunulia hivyo vitu

ngaizaskids said...

Da Ester Hawa watu wanahitaji Msaada kuna kipindi huwa kina rushwa wanaonyesha watu wasopenda kutupa vitu wana vitu kibao Hadi vyakula mpaka hawana pakupita Hadi kitanda hakionekani wanatia huruma, kuna how clean is your house now huwa wanaonyesha watu wachafu kupindukia ila kile kingine cha makorokoro nimekisahau mtu anafikia hatua kiachwa na mmewe au mkewe lakini atunze madude inaskitisha nadhani huyo jamaa anahitaji Msaada mkubwa.

Ester Ulaya said...

wengine wagumu sana kuelewa, kama huyu mzee ni mbishi sijawahi ona, lol