Friday, August 3, 2012

KUTOKA ARUSHA

Huyu trafic Arusha juzi kati alikamata bodaboda ya matairi matatu maarufu kama toyo kwa kosa la kutokuwa na namba za usajili ingawa ilionekana mpya haijatumika, basi akawashusha wale vijana akaendesha yeye, ghafla makutano ya mtaa wa bondeni akashindwa kukwepa gari dogo akaligongeza toyo kwenye gari. je sheria zinasemaje kwa tukio kama hili? baada ya muda traffic akaitelekeza bodaboda na kupanda hilo gari dogo lilionekana kupata madhara wakatokomea kwenda kumalizana. 

Pata matukio zaidi kwa picha chini


Toyo na Gari zikiwa zimegongana na aliyesababisha hii ajali ni askari
Asante sana Mdau wa Rural and Urban Blog kwa matukio haya

No comments: