Wednesday, February 22, 2012

GOOD MEMORIES @MPANDA GIRLS SECONDARY SCHOOL

Maranyingi nimekuwa na utaratibu hasa nipatapo nafasi kutembelea shule nilizosoma, Lengo ni kusalimia, kuona maendeleo na kujua Lipi linaloendelea kujiri shuleni hapo, hata ikibidi kutoa chochote nilichonacho hasa katika kuhamasisha wanafunzi wawe na moyo wa kusoma kwa bidii, Mwaka jana Nilienda kutembelea shule ya Secondary niliyosoma Form I hadi Form IV, na hii ilikuwa ni mara yangu ya 3 kwenda hapo katika nyakati/miaka tofauti tokea nimalize shule.
Jiko la Shule
Nadhani mnafahamu changamoto wanazokutana nazo wapishi wa shule zenye mkusanyiko wa wanafunzi wengi, kuna mama ni mpishi hapa, hadi leo huwa nawasiliana naye, maisha yake ni magumu sana, huwa nikienda ananipokea kwa furaha sana, kutoa ni moyo na huwa najitahidi kumsaidia kukwamua baadhi ya matatizo akutanayo nayo hasa kifedha, kidogo nilicho nacho nampa ana solve yanayomtatiza
Wanafunzi wakisafisha mtaro wa maji machafu yatokayo jikoni
Wanafunzi wakiwa busy kufua nguo zao, kwa nyuma ni Mabweni

Infirmary
School Assembly
TATA
Hili gari lipo hadi leo, na tulikuwa tunaambiwa lililetwa tokea shule ilipoanzishwa mwaka 1986
Nikielekea Duka la Shule kuongezea chochote kwa ajili ya wanafunzi
Nilipofika shuleni, nilijitambulisha kwenye ofisi ya waalimu, nikamkuta mwalimu aliyenifundisha, mara zote namkuta, ila alikuwa anawahi kwenda mjini, kwani shule ipo nje kidogo ya mji kama 4Km, walimu walifurahi, tukapiga story 2,3, kengele ikagongwa, wanafunzi wakaja Parade, Huyo dada pembeni ni Mwalimu, alisoma pia hapo mbele yangu ndo alinijuza hivyo, kwani sikumkuta wakati nasoma, alikuwa ndo mwalimu wa zamu, nikapewa nafasi ya kuzungumza na wadogo zangu, mweh mweh mweh, hiyo nafasi huwa ni ngumu, ila nilijitahidi kuwaeleza wanafunzi yawafaayo kwa wakati ule na faida zijazo baada ya shule, nikiwa nimeshika viburudisho vyao
Baada ya maongezi na wanafunzi nikawagawia zawadi za mwanzo
Pia baada ya hilo zoezi, nilipata fursa ya kuongea na wanafunzi mbali mbali, hiyo shule wanafunzi wengi wanatoka vijijini, na wanafunzi wengi kuchelewa kwenda shule wakati wa kufungua shule ni kawaida, hasa ni uhaba wa Ada na baadhi ya matumizi ya shule kupatikana huwa ni tatizo kubwa, katika walio nitouch zaidi pia kupitia msaada wa mwalimu, niliweza kufanya kitu juu yao hasa kwa muhula uliofuatia, KUTOA NI MOYO, SI UTAJIRI
Baadhi ya matokeo ya miaka iliyopita, mnapenda kujua ya kwangu hapo yako wapi? Sisi ni wale tulikatiwa mitihani wakati uleeeeeeee, kwani uliibwa mnoooooooooo, to be honest, shuleni kwetu hata haukufika,tulifurahi sana na tulitunga nyimbo za kumsifu Kapuya, kwani alitukwamua ktk range ya kufeli mno, Namshukuru Mungu nilifaulu  
Unakumbuka mambo ya shule? "nitasoma PGM niwe Rubani, mara Nitasoma PCB niwe Daktari", hapa ni Main Switch, kwa tuliosoma nao watakuwa wanakumbuka,niliwahi kupewa jukumu la kuzima na kuwasha umeme chumba hiki, Kila ikifika saa 1 kamili jioni naenda kuwasha umeme, na ikifika saa 4 kamili usiku naenda kuzima, shule inakuwa giza hasa, kwani umeme ni wa Genereta na sio Tanesco, nilipita kupaona, kujikumbusha zaidi,kwani hii kazi ilinipelekea kupenda kusoma mambo ya Umeme, hadi ilinibidi nisome PCM, leo hii nipo fani tofauti na umeme, ndoto hizi jamani
 Story za hapa na pale na walimu na wanafunzi
Nilipelekwa pia Maabara, siku hizi hii shule kuna Form V na VI, wakati twasoma siye ilikuwa ni O'Level tu
Wanafunzi wakinionyesha mambo ya maabara, nilipokelewa vizuri sana hadi raha
Dereva Sanga wa TATA, aliponiona alifurahi sana, amekuwa akiniona mara kadhaa, hajanisahau, akituchekesha hapo, ni dereva wa kitambo sana, na bado yupo hapo shule
Nikiwa Staff Room na mwalim
Msomaji wangu, mara ya mwisho ulitembelea lini shule uliyosoma? hata kama ulikuwa mtukutu vipi, unachapwa sana, wewe kipanga sana, hata shule ya msingi tu, ipo siku nitapost nilipoenda shule yangu ya msingi kubarizi na kuperuzi kijijini kwetu, mi naona ni jambo jema mno, linasababisha tukumbuke mambo mengi, pia wanafunzi wakifahamu ulisoma pale wanajua kuna ku-move forward, mwenye experience hiyo naomba atutumie kupitia ester.ulaya@gmail.com, ili watu wahamasike wawe wanafanya hivyo, hizi shule ndo zitoazo Madiwani, Wabunge, Mawaziri, Maraisi, Masurveyor, Madaktari, Waandishi wa Habari, Waalimu, Mama Lishe, Kuli,Wakurugenzi,n.k
Waalimu wakiwa wame pose ofisini kwao. Samahani post ni ndefu sana, lakini nadhani mmeweza kuipata nia yangu, tupende tulikotoka, OLD IS GOLD

5 comments:

brizzleleo.blogspot.com said...

duh inabidi namie niende kutembelea shule yangu this time ni kirudu home.

Ester Ulaya said...

Ufanye hivyo my dear, utuhadithie yaliyojiri huko na yanayoendelea

Mija Shija Sayi said...

Yaani nimeangalia picha hizi huku akili yangu ikiwa Nganza sekondari, nakumbuka tulivyokuwa tukifua, tukivusha vyakula kupeleka mabwenini, tulivyokuwa kukikimbia mchakamchaka..prepo kabla ya kulala na mengine meeengi, aiseee Esta umenipa wazo, nami Nganza nitarudi.

Ubarikiwe sana.

Ester Ulaya said...

Da Mija kumbe ulisoma Nganza? Nami nilisoma huko, siku nilipoenda wala sikuwa na Camera, nenda mamie ukaone jinsi siku hizi ni A Level tuuu, no O level tena

Rachel siwa Isaac said...

Nijambo jema kukumbuka tulipotoka,Kazi nzuri.