Monday, June 11, 2012

WANANCHI WAJITOKEZA KWA WINGI MANISPAA YA TEMEKE KUCHUKUA FORM ZA VIWANJA VYA GEZAULOLE

 Leo Manispaa ya Temeke walianza zoezi la kutoa form za viwanja vya Gezaulole,Kigamboni. Zilikuwa zinauzwa 30,000/- Tsh moja. na walikuwa wanapewa namba, unahudumiwa kwa namba kadiri ulivyowahi kuepusha uchakachuaji. Utaratibu utakaofuata ukipata kiwanja utatakiwa ukilipie ndani ya wiki 2
Walipewa eneo maalumu wapumzike wakisubiri huduma, wananchi walijitokeza kwa wingi hasa
 Kuna muda yalitokea maswahibu kidogo kati ya askari na wananchi.....baadhi ya wananchi walihisi haki haitendeki na wamekaa muda mrefu tokea alfajiri
 Wananchi waliowahi kupata form zao walijitahidi kujaza hapo hapo, kama unavyowaona hao wakijaza
 Waliokuwa na namba za mbali walikaa mbali kidogo kusubiria zamu yao ifike
 Wakiingia na kutoka ndo hali ilikuwa ni mpishano tu
Hivi kitaeleweka kweli leo?????????
 Askari walikuwa busy mnooooo
 Wananchi mbali mbali wakiwa busy...lengo hasa ni upatikanaji wa form na kujaza ili waweze kulipia viwanja wakipata
Askari wakiwajibika

No comments: