Wednesday, June 20, 2012

MARA YA MWISHO UMEENDA LINI KWENYE MASHINE YA KUKOBOA NA KUSAGA???

Mashine ya kusaga, ipo maeneo ya Kinondoni A mtaa wa Togo
Mimi mara ya mwisho nilienda jumatatu ya wiki hii nilienda...ila nilikuwa na muda mrefuu kidogo sijavisit maeneo ya mashine hizi
Hii ni mashine ya kukoboa
Kama mahindi yana vumbi sana yanachekechwa eneo hili
Shughuli ya kuyachekecha mahindi ikiendelea
Mashine ya kukoboa mahindi na inayapepeta pia, yakitoka hapo ni kusaga tu kama huendi kuyaloeka...maana wengine yakishakobolewa anayaloweka kwa siku kadhaa ndo akasage yanakuwa meupeeeee


Unga ukijaa kwenye mfuko, kilo moja kukoboa ni 150/- :Tshs na kusaga kilo moja ni 150/- Tshs

No comments: