Sunday, June 17, 2012

JUMAMOSI ILIKUWA NI SIKU FUPI SANA KWANGU

 Huku ni kwa-Tumbo Bagamoyo, nikwaonaga akina mama kama hivi natamani kila muda niwaamkie, heshima juu yao ni kubwa mnooooooooo
 Huyu mtoto alinisababisha niumie sana baada ya kuona hili kovu bado halijapona vizuri, wanasema mama yake alikuwa anachoma mabiwi shambani, akasikia mtoto analia kumbe kaangukia humo anaungua
 Na hapa bado hakijapona vizuri, ni mdogo hata bado hajajua kuongea vizuri, tuwe makini na watoto hasa kuwakinga na vihatarishi kama moto, maji,michanga n.k.
 Sasa kama hapa mtoto yupo jikoni, kidonda hakijapona na dada yake anachochea moto hajafunikwa hata nguo, nilimshauri mama mtu ajitahidi mtoto awe mbali kabisa na maeneo ya moto ili apone mapema....si mnajua kidonda cha moto kikipata joto la moto kinapata maumivu makali
Baada ya kazi iliyonipeleka wenyeji walinipa zawadi ya mahindi mabichi, ndani ya bag nyuma kuna machungwa na papai.

7 comments:

Yasinta Ngonyani said...

nimesikitika kidonda cha huyo mtoto halafu naona kama kinaanza kutunga usaa...Kutumanisha kweli unaweza eti mahindi mabichi, machungwa na papai:-)

Ester Ulaya said...

YES KINATUNGA USAHA, YAANI NAONA KAMA HAWAKIJALI, NZI WALIKUWA WANAMZONGA TUUUU.........MAHINDI YA KUCHEMSHA MATAMU, TENA YAKIWA FRESSHHHH, M NITAKUJA BUSTANINI KWAKO YASINTA...

Yasinta Ngonyani said...

Je uliwashauri vipi maana kinaweza kuoza na kuwa hatari sana...Acha bwana kuzidi kunitamanisha ..tatizo hapa bustanini kwangu mahindi hayakubali kwa hiyo sijapanda...

Ester Ulaya said...

Kuna dawa wanampa na kumpaka, nikawaambia kwakuwa hawawzi kumvisha suruali au kaptula, wajitahidi wamfunge rubega ili nzi wasishambulie kidonda kinaweza kurudi, wahakikishe haingii jikoni, wakiona usaha unazidi wampeleke hospitali tena fasta, na kwakuwa anapenda kucheza wasimuache mwenyewe si unajua tena kuku huwa wanapenda kudonoa vidonda, watamsababishia adha kubwa......hilo ndo nilijaribu kuwaeleza wakasema watajitahidi

Ester Ulaya said...

kama mahindi hayakubali, jaribu kupanda karanga na njugu...tutachemsha hata hizo...hahahahaha

Yasinta Ngonyani said...

Ester naomba kuwasiliana nawe ni vipåi nifanye hapa ni add ya mail yangu:- ruhuwiko@gmail.com

Ester Ulaya said...

ok