Saturday, June 23, 2012

GARI LA BIA LAPATA AJALI SUMBAWANGA...WANANCHI WALEWA CHAKARI

Hii imetokea leo jumamosi asubuhi majira ya saa tatu asubuhi baada ya gari ya kampuni ya Kanji Ladji inayobeba bia iliokuwa inatokea Mbeya kwenda Sumbawanga ikiwa imesheheni vinywaji kupata ajali na kuanguka majira ya saa tatu asubuhi.


 Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi.....baada ya ajaali hiyo kutokea kijiji cha Mshani km 19 kutoka Laela-Sumbawanga ilikuwa kama sherehe kwa wengine kwani wanakijiji walivamia gari na wakaruhusiwa kunywa watakavyo ila hakuna kuondoka na chupa.....asubuhi watu walikuwa wamelewa chakari...Maisha bora kwa kila Mtanzania...

Asante sana Reporter wetu Wa Rural & Urban  Kutoka Sumbawanga Veronica

No comments: