Wednesday, June 27, 2012

AJALI YA BASI YATOKEA ASUBUHI YA LEO


Bus la abiria(MUBARIKIWE)lenye namba za usajili T135ALR linalofanya safari zake kutoka Sumbawanga-Mbeya-Sumbawanga leo majira ya saa mbili asubuhi limepata ajali na kuchomoka tairi mbili za mbele.Basi hilo limegonga moja ya alama za barabari(kerbstone) eneo la Kianda kijijin kutokea Sumbawanga eneo ambalo kuna daraja namba moja linalojengwa na kampuni ya ujenzi wa barabara inayotengeneza barabara ya Laela-Sumbawanga..
 Wananchi wakiwa wamekusanyika

 Chanzo cha ajali hiyo  ni mwendo kasi wakati basi halina brake pia uzembe wa dereva umechangia asilimia kubwa kwakuwa alikuwa overspeed katika mteremko ambao mbele kuna daraja na Bahati nzuri kuna mashine inayoitwa bulldozer ikasaidia kuizuia isitumbukie mtoni kama picha inavyojieleza..Kama haitoshi huo ubichi karibu na basi ni mafuta ambayo yalitaka kusababisha kulipuka kwa basi..


 Mpaka tunatoka eneo la tukio hakuna abiria yeyote aliyepata matatizo na polisi wa usalama barabarani kituo cha Mpui walikuwa ndo wanaelekea eneo la tukio.



 Ikumbukwe kuwa mwendo kasi katika barabara inayotengenezwa ni hatari kwani haijapita hata wiki moja ambapo gari ya kampuni ya Kadji Lanji inayobeba Bia kutoka Mbeya kuja Sumbawanga nayo ilipata ajali na kusababisha hasara kubwa ambapo mpaka sasa dereva anashikiliwa na jeshi la Polisi mkoa wa Rukwa.
Shukrani sana Reporter wetu wa Rural & Urban Veronica kwa habari hii

2 comments:

emuthree said...

Kila mara ikitokea ajali ni usemi ule ule wa mwendo kasi...na utaona mgari /mabsi yakifukuzana mabarabarani huku tukishangilia,...

Ajali haina kinga,lakini mengine tunajitakai wenyewe, hivi tukiamua kwa pamoja, kama dereve anaendesha kwa mwendo kasi, kuwa sifanye hivyo tutashindwa?

Interestedtips said...

emu-three ulichosema ni sahihi kabisa mpendwa, hivi siku madereva wakiamua kuwa sasa umakini uwepo na mwendo kasi upungue nina uhakika Kinga itakuwa imepatikana na zitapungua kweliii