Monday, May 21, 2012

TUONGEZE UMAKINI BARABARANI

Hii imetokea asubuhi ya leo maeneo ya salenda, school bus hii ilikuwa mbele yetu tena imebeba wanafunzi, mara tukaona imepanda hapo juu, sasa sijui ni ubovu wa gari, au alikosea mahesabu, au mawazo yalikuwa mbali, cha kwanza niliwaza hao watoto waliobebwa maana walikuwa wanapiga kelele, bahati nzuri halikuanguka akarudi nyuma kujikwamua hapo juu akaendelea na safari.

Ikiwa ni mwanzo wa wiki, nawatakia kazi njema na mlio mashuleni shule njema, mlio majumbani nawatakia shughuli njema za hapo home. 

3 comments:

Simon Kitururu said...

Nakutakia nawe Wiki njema Dada yangu!

Na kweli tujihadhari!Yani na nyie mngekuwa spidi si ingekuwa ishu?

Ester Ulaya said...

SIMON YAANI INGEKUWA NI BALAA

ASANTE SANA

Majoy said...

Mungu atulinde tu huko mabarabarani maana nihatari sana