Saturday, April 14, 2012

WAKATI WA KUVUKA BARABARA


1. Usisimame au kucheza bara barani.
2. Kabla ya kuvuka barabara, simama angalia kulia, kushoto, halafu kulia tena kama hakuna gari, vuka moja kwa moja mpaka ukingo wa pili wa barabara.
3. Vuka barabara haraka lakini usikimbie; vuka barabara kwa tahadhari kubwa. Kama karibu yako kuna vivuko vya waenda kwa miguu yaani mistari ya pundamilia (zebra crossing) vitumie.
4. Zingatia ishara za taa za barabarani, ishara za maelekezo ya polisi na michoro ya barabarani. Maelekezo ya askari Polisi ndiyo yapewe kipaumbele.
5. Chukua tahadhari kubwa ikiwa huwezi kuona vizuri kwasababu ya magari yaliyosimama au vitu vingine vinavyokuzuia kuona vizuri barabarani.
 NI KATIKA KUKUMBUSHANA TU, KWANI AJALI HAZIJAISHA NA ZINATOKEA KILA MARA
MUWE NA WEEKEND NJEMA WADAU WANGU, MIMI PENDA NYIE SANA

No comments: