Thursday, April 12, 2012

UGALLA RIVER - MPANDA

Unafahamu Ugalla River? Hizo ni baadhi ya picha zikiuonesha mto Ugalla ambao umekuwa ukikauka siku hadi siku.zamani kulikuwa na imani kwamba mto huo ni wa mizimu hivyo unaweza pita hapo mkamuona mwenye mto akitokea katikati ya maji na kuomba lifti ya treni na mkimyima basi treni haiondoki, hizo ni story za zamani.…na kwamba kupita hapo bila kutoa sadaka basi mnaweza kukwama na watu kwa imani hiyo wakawa wanatupia hela za kichele ili wavuke mto huo salama..Imani hiyo ipo mpaka leo kwa baadhi ya watu kwamba wakipita lazma watupie sadaka kwa mzimu wa mto huo lakini cha kushangaza baadhi ya watoto wamekuwa wakisubiria pembeni ya daraja la mto huo ili wewe unapotupia sadaka yako kwa mizimu basi wao wanaokota......…HIZO NDO IMANI. TUBADILIKE,




Asante sana mdau wetu Veronica kwa maelezo hayo juu na matukio ya picha

No comments: