Friday, April 13, 2012

MWAKA 2007 NILIWAHI KUMPONGEZA MAREHEMU KANUMBA KWA KAZI ALIYOKUWA ANAIFANYA

Kutoa pongezi kwa mtu anayefanya kazi vizuri na ukaguswa ni 

jambo jema sana. Nakumbuka kipindi kile cha maigizo ya 

Runingani ya Kaole Sanaa Group nilikuwa mfuatiliaji sana  wa 

maigizo hayo hadi walipohama ITV wakawa wanaigiza TVT kwa

 sasa ni TBC. Nilipenda uigizaji wa Kanumba, walipoanza 

Tamthilia mpya iitwayo TETEMO Kanumba hakuwepo kwenye 

hilo Igizo, kwakuwa nilikuwa naipenda kazi yake, nilimsaka, 

ilikuwa July 2007, kwanza nilimpongeza kwa kazi yake, then 

nikamuuliza kwanini haigizi tena, aliponijibu.., nikamuuliza 

movie 

alizifanya muda huo, Kijana wa watu hakuwa na HIYANA 

alinijibu vizuri tu, hapo alidhihirisha si mtu wa majivuno. 

Nimejaribu kuweka email hizo hapo chini uone ilivyokuwa. 

NIMEJIFUNZA KUWA, UNAPOONA MTU ANAFANYA VIZURI MUELEZE MAPEMA AJUE, TUSISUBIRIE HAYUPO, MTU AKIELEZWA MAPEMA ANAFARIJIKA NA  ANAONGEZA JUHUDI ILI ANAPOHARIBU APAWEKE SAWA, NA ENDAPO SIFA ZIKIMZIDI IKAFIKIA ANAHARIBU AELEZWE PIA KWA LUGHA NZURI NA SIYO YA KASHFA AU HATA MATUSI, LENGO NI KUTHAMINI KAZI YAKE NA MCHANGO WAKE KATIKA JAMII. NA WENGI TWAJIFUNZA KUPITIA MAZURI HAYO

 Tarehe 15 June 2011 ilikuwa ni siku ya Kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Jide, ndio ilikuwa mara yangu ya mwisho kumuona kwa ukaribu zaidi, kwani alikuwa amealikwa pia kama mimi kwenye Party hiyo
MAADAMU MAREHEMU KANUMBA ANGEAMKA GAFLA SIKU YA MSIBA WAKE AKAKUTA WATU WANVYOMLILIA ANGEZIMIA KWA FURAHA

 Alichokuwa ananifurahisha zaidi huyu Kijana ni juhudi zake, na kusemwa kote vibaya hakukata tamaa kuipeperusha bendera yetu, alikuwa anachanja mbuga nchi mbali mbali, vijana wengi wamepata ajira za kudumu kupitia yeye, hatuwezi sema tuko perfect 100%, kila binadamu ana mapungufu yake, anaweza kuwa alikuwa nayo, lakini mazuri yake ndio twayahitaji na tuyabebe kumuenzi. Naamini wapo waliokuwa wanamsfia na kumpongeza wakati akiwa hai na alisema Asante, ila kwa jinsi binaaadamu tulivyoumbwa ukiambiwa baya lako linauma na unasononeka, ndo tumeumbwa hivyo hatuwezi kuikwepa hiyo hali hata kidogo. 
Ushauri wangu kwa Waigizaji : Fanyeni kazi yenu kwa bidii, fundisheni Tanzania maadili kwenye Movie zenu, muienzi asili yetu ya Tanzania, muwe mifano ya kuigwa kwenye jamii yetu, unganeni pamoja kutetea haki zenu, kuweni wabunifu kila mara umizeni vichwa ili Watanzania wasizichoke kazi zenu, hudhurieni Course mbali mbali zihusuzo kazi zenu ili muweze kwenda na wakati. Nimalizie hapa kwani ninayo mengi sana yakuongea juu yenu ili tuifurahie zaidi kazi yenu
RIP THE GREAT TUTAKUKUMBUKA DAIMA

1 comment:

kokusimah said...

Ni kweli dada tuwaambie watu mapema kwani wakishakufa ndo imekwisha, Nami nayo furaha nilimwandikia mwezi Jana na namshukuru Mungu nililisema nililokuwa nalo na sasa najisikia safi kafa ameliona. Juzi nilimwambia kaka Kama Kanumba angestuka Akaona watu tulivyompenda agekufa kabisa kwa mshituko. Apumzike salama.