Thursday, March 22, 2012

MGAO UMEANZA KIMYA KIMYA NADHANI HASA BAADHI YA MAENEO DAR

Kuna baadhi ya maeneo Dar umeme unakatika mara kwa mara, inaashiria kuwa mgao umeanza au kuna marekebisho yafanyikayo bila wananchi kujua hilo. Lakini kwakuwa inatuathiri sana tunajitahidi kutafuta njia mbadala ili mambo yetu yaende sawa na yasisimame. Jana usiku nimeweza kushuhudia tukio lililokuwa linaendelea bila kujali umeme utarudi muda gani, kwani njia mbadala zilitumika hasa kuwasha taa za solar
Jengo la Tanesco Ubungo
Umeme ukukatika yatubidi kutumia Chemli, ingawa wataalamu wanashauri kuwa moshi wake kiafya si mzuri
Mama alikuwa busy anapika akiwa kawasha taa yake ya solar, hii ilikuwa jana usiku, hiyo taa ya solar kaielekezea jiko lilipo, wengine tulikuwa pembeni gizani kwakuwa hatukuwa na taa nyingine
Ni giza ndiyo, lakini angalia kwa umakini zaidi utaona kuna ndoo, sinia, masufuria na vifaa vingine vya jikoni
Hata mkate umeme miaka yote tutapika tu, mama yuko busy anapika
Hapa akiwa mlangoni anatoka ndani akiwa kashika taa yake
Shemeji yake alimsaidia kushika taa,akaielekeza kwa chini, gafla wakamwambia kwanini unaelekeza chini? weka mezani imulike pote
Taa ikapelekwa mezani, makaratasi yakawa yanasomwa na watoto kama kawaida yao kuizunguka meza kuangalia yanayojiri
Kuandika andika kukatawala
Hata umeme ukikatika pesa zitahesabiwa tuuu, hata kwa torch
Taa ya  Solar ilifanya kazi kubwa, si unaona wanajitahidi kusoma kilichoandikwa
Mpaka hapa nimehesabu ni kiasi kadhaaaaaa
Sasa Tanesco twaomba sana muwe wazi, kwani wafanya biashara wanaadhirika na kukatika katika kwa umeme, wananchi tuishio seheme umeme ulipo tunapata shida, tumezoea umeme, fridge zinakuwa makabati ya vyombo sasa, vifaa vingi huwa vinaungua kwa kurudi na kukatika umeme ghafla, tufikirieni, toeni taarifa wananchi tujue na tuwe tayari.

ANGALIZO: Picha ni nyeusi kwakuwa zimepigwa umeme ulipokatika, kukawa ni giza, hivyo kuonekana sehemu zenye taa tuu, uangaliapo, check kwa makini utaweza kuona baadhi ya vitu

2 comments:

kokusimah said...

Nilalapo nakuota wewe, niamkapo ni kheri mama wee, Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote, inauma kwa kweli.

Interestedtips said...

siasa yakoooo na desturi....................
kuimba raha, utekelezaji sasa