Maelfu ya Wafaransa wameandamana katika
barabara za mjini Paris kupinga mpango wa serikali kuhalalisha ndoa
kati ya jinsia moja.
Mswada uliopendekezwa na serikali ya kisoshalisti ya Francois
Hoillande itaruhusu watu wa jinsia moja kuoana na kulea watoto.
Watu kama laki moja wameandamana katika mihadhara mitatu tofauti
na kukusanyika karibu na Eiffel Tower.
Waliotayarisha maandamano hayo wanasema waliohudhuria ni nusu
milioni.
Watu walitoka sehemu mbali-mbali za nchi kwa mabasi maalumu
yaliyokodiwa pamoja na treni kwa sababu wanaona mpango wa serikali
kuhalalisha ndoa kati ya watu wa jinsia moja na kulea watoto,
utaharibu msingi muhimu wa jamii.
Bunge linatarajiwa kujadili mswada huo baadae mwezi huu.
Maandamano yanaungwa mkono na kanisa la Katoliki na upande wa
upinzani wa mrengo wa kulia.
Lakini wasemaji wanashikilia kuwa maandamano hayo siyo ya kisiasa
wala ya kidini na wala hayawalengi wapenzi ya jinsia moja.
Maandamano hayo ni upinzani mkubwa kabisa dhidi ya Rais Hollande
tangu kuingia madarakani mwezi wa May.
No comments:
Post a Comment