Wednesday, October 17, 2012

ZAIDI YA WANAFUNZI 300 WA SHULE ZA MSINGI ZA DAR WASHIRIKI ZOEZI LA KUNAWA MIKONO.

Mgeni rasmi ambaye ni Mratibu wa Tiba wa Manispaa ya Kinondoni, Sirila Mwanisi akizungumza katika maadhimisha ya Siku ya Kunawa mikono katika viwanja vya Posta, Kijitonyama, inayofanyika Oktoba 15, huku kwa wanafunzi hao wakiadhimisha jana katika viwanja hivyo.
Wanafunzi ya 300 kutoka shule za Msingi Shikilango, Kijitonyama Kisiwani, Mapambano, Mwangaza na Mwenge wakionyesha mfano wa kunawa mikono mara baada ya kupewa somo.
Wanafunzi wakitoa show mara baada ya somo kuwakoloea.
Mwanafunzi wa shule ya Mwenge akimuonyesha mwalimu wake (aliyeshika jagi) namna alivyofundishwa kunawa mikono.
Mwanafunzi akiwadhibitishia somo limeingia waalimu wake ambao wao walichukua jukumu la kummwagilia maji.
Somo la kunawa mikono likiendelea kudhibitishwa kwa vitendo na mwanafunzi wa shule ya msingi Mapambano.
Walimu wakuwa na baadhi na wanafunzi wa shule nne za msingi zilizohudhuria maadhimisho hayo.
---



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WANAFUNZI zaidi ya 300 kutoka shule nne za jijini Dar es Salaam, jana ziliadhimisha Siku ya Kunawa mikono katika viwanja vya Posta, Kijitonyama, inayofanyika Oktoba 15, huku kwa wanafunzi hao wakiadhimisha jana katika viwanja hivyo.
Wanafunzi hao walikutana katika viwanja hivyo kuanzia saa nne za asubuhi, huku mgeni rasmi akiwa ni Mratibu wa Tiba wa Manispaa ya Kinondoni, Sirila Mwanisi.
Katika maadhimisho hayo, wanafunzi hao walifundishwa jinsi ya kukabiriana na uchafu wakati wote, sambamba na unawaji wa mikono kabla na baada ya kula.
Akizungumza katika viwanja hivyo jana, Sirila alisema kwamba ni vyema watu wakajenga utamaduni wa kujitunza kwa nyakati zote, ili wakabiriane ba maradhi yanayoweza kuepukika, vikiwano vijidudu vinavyosababisha magonjwa ya tumbo na kipindupindu.
Alisema kwamba watoto wadogo ndio wapo kwenye hatari zaidi, hivyo ni lazima wazazi na walezi pamoja na jamii husika kuwaelimisha kwa ajili ya kuwaweka katika mazingira mazuri.
“Watoto lazima waelimishwe namna ya kunawa mikono kabla na baada ya kula, maana ndio nafasi ya kukabiri vijidudu vya aina mbalimbali, ukiwamo ugonjwa wa kipindipindu ambao ndio hatari zaidi ndani na na baadhi ya nchi za Afrika.
“Serikali kwa kushirikiana na asasi mbalimbali tunaamini tutafanikisha usafi wa unawaji wa mikono kwa ajili ya afya njema, ukizingatia kwamba ndio njia ya kufanikisha maisha bora kwa namna moja ama nyingine, hasa wote tukiwa na afya njema,” alisema Sirila.
Maadhimisho hayo ya siku ya kunawa yameandaliwa na Kampuni ya PCB WITNA na kudhaminiwa na sabuni ya Protex kwa ajili ya kukutanisha wanafunzi wa shule za Msingi Shikilango, Kijitonyama Kisiwani, Mapambano, Mwangaza na Mwenge.

1 comment:

ray njau said...

Hii ni tabia njema!!