Monday, September 24, 2012

LEO UMETIMIA MWAKA TOKEA TUFUNGE NDOA: ASANTE MUNGU KWA BARAKA ZAKO NA TWAOMBA UTUONGOZE ZAIDI

 Sasa umetimia Mwaka tokea tuanze maisha ya kuishi pamoja
 Shukrani ziende kwa Mwenyezi Mungu
 NAMPENDA SANA MUME WANGU
 MR. & MRS. CATHBERT ANGELO 
 Naamini Milima na mabonde tutayavuka hadi Mwenyezi Mungu atakaposema ya kwake
 Alituachia Amri Kuu ya Mapendo, inatupasa kuendelea....palipo na upendo kusikilizana kupo, kufundishana kupo, kurekebishana kupo, kuburudishana kupo, nk.
 Siku zote 2 si sawa na 1, sijutii kuwa ndani ya Ndoa
Mungu ni mwema siku zote.......Namtja sana Mungu kwani ndiye ametuweka hadi leo na Mema yote twayategemea kutoka kwake.

MUNGU AWE NASI DAIMA ........AMEN

10 comments:

Majoy said...

Hongereni sana Mr & Mrs Cuthbert Mungu azidi kuwaimarisha katika upendo na amani.Happy 1st Anniversary dearest friend.

Ester Ulaya said...

shukrani sana Majoy....Amen

Yasinta Ngonyani said...

HONGERENI SANA TENA SANA SANA NA MUNGU AZIDI KUWALINDA NA NDOA YENU IDUMU.

Ester Ulaya said...

Asante sana Dada Yasinta

CATHBERT ANGELO said...

Asanteni sana ila Maombi yenu ni muhimu sana ili tuzidi kusonga mbele.

Mija Shija Sayi said...

Mwaka tayari...!!! Aisee siku zinaenda haraka sana. Hongereni sana kwa kutimiza mwaka, na ninawatakia maisha mema yenye YESU ndani yake.

Ila Ester naomba ufute huo usemi wa mabonde na milima, usikubali kuuweka akilini, shetani ata take advantage halafu atakusumbua sana kama akigundua unaangalia maisha kwa mtindo wa "milima na mabonde".

Kingine, kama kuna jambo unapenda Mungu awaondolee au awatimizie katika maisha yenu, njia ni kumsifu Mungu, tengenezeni tabia ya kumsifu Mungu kila wakati, ukiwa unapika, unadrive, unatembea, au unafanya chochote kile wewe ongea na Mungu, piga naye stori kama vile unamuona, mwambie yaani baba wewe ni kiboko ya dunia, nani kama wewe? ajitokeze basi kama yupo..ona jinsi ulivyotengeneza hewa, mvua, miti, usingizi... hivi kuna kinachokushinda wewe..?? na kama kipo basi kijitokeze tuone..

Halafu igeukie hiyo milima na mabonde iambie hivi nyie milima na mabonde mnaweza kusimama mbele ya Mungu wangu? kama mnaweza endeleeni..
..baada ya hapo wewe endelea kumsifu Mungu kwa kila kitu kinachokujia mawazoni. Nakwambia utaona..
Mungu anapenda kusifiwa kwa uweza wake..

Na hii si kwa Mungu peke yake hata kwetu sisi, mtu anapokusifu unakuwa mwepesi zaidi kumsaidia kuliko yule anayetaka kusaidiwa kwa nguvu...

Hata kwa mumeo pia tumia njia hii..maisha yatakwenda kama unamsukuma mlevi..

Baraka kwenu wote...

Majoy said...

Amen dear tunawaombea sana....upendo ndio ngao ya mamboi yote ktk ndoa mzidi kubarikiwa.

Ester Ulaya said...

Da.Mija shukrani sanaaaaaaaaaa......yaani maneno yako ni matamu mnoooooo, mazuri na yanaeleweka......tutazidi kuyafanyia kazi daima ...Amen

Disminder orig baby said...

Kweli Mungu ni mwema.
Mwaka umekwisha kama jana.
Hongera sana, na Mungu azidishe amani zaidi katika nyumba yenu. Amin

clicksomemore said...

Hongera Esther n hubby