Sunday, July 22, 2012

FUNDISHO SIKU YA JUMAPILI YA LEO

Padri mmoja mzee alistaafu na wanaparokia walimfanyia sherehe kubwa. Katika sherehe hiyo, mbunge wa eneo hilo alipangwa kutoa hotuba ya shukurani ya kumuaga padri huyo kwa niaba ya wanaparokia wote. Bahati mbaya, mbunge alichelewa kufika .

Mc akamwomba padri aseme machache wakati wanamsubiri mheshimiwa mbunge.


Padri hakujipanga kusema kitu lakini kwa kujitahidi, aliongea.


"Wapendwa, naikumbuka sana siku nilipofika katika kanisa hili kwa mara ya
kwanza, ila nilipata mshangao siku nilipoanza kuungamisha. Mtu wa kwanza
kabisa kumuungamisha alinishangaza sana. kwani alisema amemwibia bosi wake TV, amemwibia ndugu yake pesa za urithi, amezini na jirani yake, na pia
katembea na house girl wake. Nikapata picha kuwa kumbe watu wa kanisa hili
ndivyo walivyo, nikasikitika sana. Kumbe nilifikiria tofauti. Kwani baadaye
nikakuta kumbe watu wa hapa ni wazuri sana na hawatendi dhambi mara kwa mara na ni wastaarabu sana".

Mara mheshimiwa mbunge akawasili, padri akakatisha maongezi na mbunge
akaanza kuhutubia. "Ndugu wapendwa, naomba mniwie radhi kwa kuchelewa kwani nilikuwa na majukumu makubwa ya kiserikali. Pia ninayo furaha kubwa kwa kunipa nafasi hii kuhutubia kwa niaba yenu. Mimi nina bahati sana kwani
padri huyu alipokuja hapa, mimi nilikuwa mtu wa kwanza kwenda na kuungama
kwake...

Fundisho-tuwe tunawahi

No comments: