Sunday, May 13, 2012

MVUA ZA LEO MAENEO YA BAGAMOYO VIJIJINI

 Bahati mbaya au nzuri tulikoenda leo hatukuwa na mwamvuli, ikabidi tu niombe huu mfuko wa sandalusi walau nijisitiri nisilowane sana,baadae mvua ilipungua yakabaki manyunyu, na inabidi safari iendelee, hadi kufika tuendakonikawa nimeloana kiwiliwili,kichwa kikawa na uafadhali
 Safari ikiendelea
Barabara tope hasa
Haya ni maeneo ya Makongo mchana wa leo

9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nimeupenda mwavuli wako mdada!!

Mija Shija Sayi said...

Yaani hilo jina la Sandalusi limenikumbusha mbali saaana....Yaani Ester umenichekesha sana, nakumbuka kwetu sasa...looh!!!

Ubarikiwe dada mdogo.

Unknown said...

Pole dia ila nakupenda kwa jinsi unavyoipenda kazi yako safi sana zidi kubarikiwa.

Interestedtips said...

majoyy asante mpenzi, Da'Mija yaani hata mimi nilipoambiwa chukua sandalusi, nikakumbuka kijijiniiii, hahahahaha Yasinta yaani huo mwamvuli ulinisaidia nywele hazikuloana

kokusimah said...

Ehehe aisee huyo alokujali Na mwanvuli anajali sana manake mwanamke unywele sijui ingekuwaje, vipi kamera nayo imepata?? Kweli neno sandarusi limenikumbusha mbali hasa enzi za dodoki mh! Asante kujali mamii

Mija Shija Sayi said...

@Ngaizaskids.. unazidi kunimaliza jamani... 'enzi za dodoki' nayatamani sana maisha yale...

Interestedtips said...

hahahahaha mmenikumbusha dodoki jamani, lol

kokusimah said...

Ahaha full kutakata na mwili unang'aa km shilingi ya Nyerere ahaha ndo kwenda na wakati huko kunatutesa sana mpenzi.

kokusimah said...

Ndiyo my wii yaani enzi zile ukishamaliza kuoga na kandambili zimetakata unakiwala na kandambili zako unasepa Ahhaa uwiii ngoja ncheke kihaya mie