Wednesday, May 23, 2012

KUTOA NI MOYO SI UTAJIRI

 Kikubwa katika maisha yetu ni kumshukuru Mungu kila siku kwa kila kitu, yeye ndo anayetupa pumzi na uwezo wa kutambua na akili ya kujua namna ya kutatua matatizo yanayotukumba. Nikiangalia picha hizi napata mambo mengi sana kupitia maisha yetu haya. Kuna ambao kupata mlo kwa siku ni issue, kuna ambao kwa kulala tu mashikoro magene, kupata mavazi inakuwa ni ngumu sana
 Wapo ambao kila siku wanabadilisha nyumba watakazo, chakula watakacho, kila siku nguo mpya wanavaa, sio kwamba hawa hawapendi maisha mazuri kama wengine, ila nafasi hiyo hawana, Nani wa kulaumiwa?????????? hali hii huwa nikiifikiria nakuwa mnyonge sana, napenda kutoa wito, kwa yeyote anayeguswa kwa namna yake na una nafasi jaribu tu kusaidia hata asilimia 2 ya mapato yako, kwani inafariji sana unapoona jami kama hizi zinasaidwa
Wapo wengine kazi zao ni rahisi sana, kwa siku anaingiza millions of money, lakini wapo wanaofanya kazi ya kilimo tena cha mikono, huu ni mfano tuu, siwezi kutaja kazi zote, leo nimeguswa sana, na nikawaza mengi mnoooooo, bila kupata majibu. Lengo kuu ni kuhamasisha wenye navyo kusaidia wasionavyo, asilimia kubwa hakuna anayependa kuishi hivi ni nafasi yao inawafanya kuwa hivi. 

NB. Kila huduma ya jamii niifanyayo katika kusaidia siyo lazima niionyeshe jamii nilichofanya, tenda wema uondoke zako usingoje shukrani, na huduma zingine za jamii siyo lazima utangaze kila mtu ajue umemsaidia nani na ni kipi umempa, au mwingine anajisifia kabisa 'bila mimi yule asinngekuwa alipo' sidhani kama ni vizuri kufanyiana hivyo. Simaanishi kwamba ndo muache kutangaza mmewasaidia wangapi na kipi mmewapa, ni mtazamo wangu tu, na baadhi ya mafundisho niliyoyasoma

Muwe na siku njema

SAMAHANI NILIKOSEA KUTYPE HEADING, NIMEREKEBISHA NISAMEHENI PLEASE

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hujaguswa peke yako Ester..huwa kila siku najisemea mwenyewe kwanini nina magauni kumi wakati navaa moja tu..na wakati mwingine hana hata moja..huwa nawasikia watoto wakisema mimi sitaki kula chakula hiki kwani sikipendi au si kitamu wakati wengine hawana hata hicho kisichokitamu. Lakini pia kuna jambo moja nimesikia na kujifunza ni kwamba kama unawaza hivyo kila wakati hiyo pia ni dhambi..na unapowakaripia watoto wanapata shida kujua wafanye nini je wale au wawape wasionacho na wao kukaa njaa? Hapa kunachotakiwa na kuwahamasisha hao watu nini sha kufanya kwani ukiwapa kitaisha leo hii na kesho watakuwa hawana tena... Sio kwamba nakataa tusiwasaidie ila tu hiccho kitu kiwe cha kudumu..Tenda wema nenda zako

Interestedtips said...

Maneno yako yamenigusa Yasinta, ila kama kuwaza hivyo ni dhambi kutokana na wanvyosema basi hiyo dhambi nimeshaitenda sana tena kila siku, Mungu ninusuru hayo mawazo yasije sana, asante kwa mchango wako wenye nguvu

kokusimah said...

Hiki kitu ndo taabu ya moyo wangu, nateseka sana na kuwa za watu hawa, na zamani
Nilikuwa nawaza Nina shida bila kuwa za kuna wanaonizidi ee Mungu atulinde na atupe mioyo
Ya kusaidia.

Asante mami umenigusa kwenye kidonda.

Interestedtips said...

Pole sana my Wii