Thursday, May 3, 2012

THE EASIEST DIET EVER: MOST EFFECTIVE & EASIEST TO FOLLOW

Naomba leo niweze kushare na wale waliopenda niwaeleze diet iliyonisaidia kutoka 68kg hadi sasa nina 61kg.
katika maisha ya kawaida kabisa hasa siye wabongo nimegundua kuwa ni ngumu sana kufuatilia diet zile zenye ratiba kali ambayo ni lazima ufanye mazoezi ili ugain mwili utakao na uupate uzito utakao. Nilishawahi kujaribu sana hizo lakini mwisho wa siku najikuta nacheat, halafu najipa moyo kuwa kesho sitocheat.

KUNA WENGINE NI WEMBAMBA HATA WALAJE WANAKUWA HIVYO HIVYO WENGINE NI MAUMBO YETU JINSI UNAVYOKULA NDO MWILI UNAGAIN, JIFAHAMU UMBO LAKO ITAKUSAIDIA

Nilijaribu kufuata utaratibu ambao sitoumia hasa kutokana na upatikanaji wa mahitaji ya msosi kwa urahisi na diet nifanyayo isiwe ngumu mwisho wa siku nikashindwa kufanikiwa, ila kwa sasa nimestop kufanya mazoezi kwa muda sina sababu ya muhimu, ni uvivu tu, nilipoona nilacho hakininenepeshi sana nikajikuta sifanyi zoezi.

Diet yangu nilikuwa nazingatia nilacho, na sikuwa na ratiba ya kuwa j tatu nile nini au j4 nile nini,hiyo yote ni katika kujifariji na kuogopa kucheat, samahani kwa maelezo marefu, lengo ni mulielewe nini najaribu kuelezea.

MAMBO YA MUHIMU NILIYOZINGATIA NA AMBAYO NAPENDA UZINGATIE UKIIPENDA DIET HII.
a) Niliacha kutumia sukari
b) Soda/Juice za kopo au box nimepunguza kabisa kutumia, ukiona nimekunywa hivi vitu basi ujue nimealikwa sehemu nikanunuliwa maranyingi naomba maji kukwepa hilo.
c) Red meat naikwepa mnooooooooo, ni shughuli hapa nipendavyo nyama mie nk.

IPO HIVI, NA NAJITAHIDI IENDELEE HIVI, KWANI MAANA YA DIET SIYO UPUNGUE KILA SIKU, ILA WAWEZA MAINTAIN UZITO UUPENDAO UBAKI HIVYO HIVYO ILA ZINGATIA ULACHO
Mara nyingi nikiamka asubuhi kabla ya mswaki nakunywa maji, hii nimemuambukiza hadi Mr. naye kaanza kujifunza tararatibu, ni ngumu kuyazoea, fanya hivyo, faida yake nilishaielezea post ya nyuma
Huwa najitahidi nakunywa kikombe kimoja cha chai, naweka Mchai chai, unasafisha damu,tafuteni kazi yake mtajua, halafu badala ya sukari naweka asali, ninayo asali Original ya kutoka Tabora, naipata kwa urahisi mno, siku nikiwa naagiza nitawajuza, atakayetaka tuwasiliane
Nimeizoea sana asali, hata nikitengeneza juice najiwekea asali, sukari siipendi tena
Sasa hiyo chai itategemea na siku, naweza nikaishushia na vipande viwili vya mkate au mayai mawili ya kienyeji ya kuchemsha, naoga then job, sasa hapa usijishindilie meeeengi wakati wa chai unakomeshea, chapati,supu,maandazi,chips(wapo walao chips asubuhi), hapa kila asubuhi waweza badilisha bites,ila zisizidi 2 tu
Maranyingi najitengenezea matunda naenda nayo job, mwanzoni utaona usumbufu ila utazoea, ikifika mida ya saa 4, napiga matunda yangu

Sasa muda wa Lunch ndo kimbembe kilipo, kuna siku naagiza kipande cha kuku na viazi viwili vya kuchemsha kama picha hapo, siku zingine naagiza samaki tuuuuu na kachumbali, siku nyingine firigsi tu na kachumbali, au naagiza ndizi 2 za kuchoma tu na kachumbali, mchana najitahidi sana nisile wanga mwingi na nisishibe sana, sehemu kubwa inakuwa ni maji na matunda
Jioni na siku za jumapili huwa kidogo najiachia, nakula pilau kama hivi ila kwa kiwango kidogo kama huwa unajaza sahani sasa hivi iwe nusu, wanga mwingi mwilini ndo unasababisha mwili unenepe na mafuta, mie napikiaga mafuta ya Alizeti hayajachakachuliwa
Siku zingine jioni najilipua na mchanyato wa viazi,njegere,sosage, nyanyachungu kidogo, ila sijazi hivi sahani huo ni wa Mr.
Kuna muda unatingwa, nashindwa kutoka na matunda home, nanunua kama hivi
Haya nilitengeneza nikabebamwenyewe,kwakuwa bakuli linakuwa limejaa matunda nikila hiyo saa 4, yanabaki, nayala tena saa 9 wakati wa kukaribia kutoka job,luch huwa ni saa 6 na nusu hadi 7 na nusu najitahid niwe nimekula
Kama hivi, siku nyingine nikabeba ya aina hii
Kuna muda nachelewa kuamka nakosa muda wa kuyaandaa, nayasafisha nabeba hivi, job kuna kisu
Chips natengeneza mwenyewe siku nikiwa na hamu, hapo ni jioni nimepika kisamvu cha kuchemsha nikakatia carrot, ndo nikala hivyo
Maji zingatia sanaaaaaa, mimi hadi muda wa kwenda kulala huwa nimekunywa kwa siku lita 3 au na zidi, huwezi kuyanywa yote kwa mpigo, yape interval, ila usinywe wakati unakula, ukimaliza kula tulia kwa muda ndo unywe
Siku zingine napika kisamvu cha karanga, na bamia na wali kidogo. Yote hii ni kutokana na mazingira nishiyo, kwa wale wanaoweza kufuatilia zile ratiba fanyeni mimi hii imenisaidia na nimepungua kutoka 68kg had 61kg, usile msosi mwingi kama mashindanoni, tumbo litazoea tuuuuuu

ANGALIZO: Usishinde bila kula kwani utapungua vizuri, ila unakaribisha magonjwa yatakayokupa shida, kula ni muhimu. Kwa wale wanandoa ukishinda bila kula na jioni ule kiduchu, unaweza kuzimia wakati wa kujig jig hahahahaha, utakuwa huna energy jamani, nafuu mchana ule kiduchu ila jioni ule walau vizuri, pia unaweza kosa nguvu hata utendaji kazi ukawa hafifu. Mboga za majani kula sana, mimi huwa ni mvivu hapa ila ikibidi nakula mara moja moja


WAPENDA POMBE JARIBU KUSTOP KWA MUDA, INANENEPESHA HASA MATUMBO, MIMI HUWA SITUMII KABISA

Tumbo ni gumu sana kuwa Flat kwakufanya diet ya msosi tuuuuu, labda kama kua kifaa maalumu cha kutumia kama vya wazungu, nashauri ufanye mazoezi ya kupunguza tumbo pia, kwani nami nina mpango wa kufanya hivyo

ALL THE BEST, FANYA KILE UWEZACHO, USICHOWEZA WAACHIE WAWEZAO WAHANGAIKE NAVYO
WAPO WASEMAO JIONI HUTAKIWI KULA KABISA, MIMI SIWEZI

AFYA KWANZA, VINGINE VISAIDIZI  TU, UKIZIDIWA FUATA USHAURI WA DAKTARI

Mafuta yasiwe mengi, ukipika chakula cha kuweka karanga au nazi, usiweke tena mafuta

KULA QUALITY NA SIO QUANTITY

Mimi penda nyie sana


11 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nimependa hii maana ni kweli sasa unaanza ule msimu wa kujiachia..LOL Ahsante sana kwa mfumo huu...TUPO PAMOJA DADA YANGU

Interestedtips said...

Yasinta umeonaeeeee yaani vyakula vitamu sanaaaaa, halafu tunajisahau, pamoja sana na Asante sana

Unknown said...

Nimetamanije hicho Kisamvu cha karanga??? ......

Jana ★ said...

Very healthy :)
Un besito ^^
http://janakitchen.blogspot.com

Rachel Siwa said...

Ahsante sana Ester, Ngoja nami nijaribu.

wise monica kaaya said...

Hahahahahaha kunamahala pamenichekesha sana asante sana

Interestedtips said...

Hahaha Wise umeona eeeeeee

wise monica kaaya said...

Hahahaha umeamua kutuvunja mbavu lol

Mija Shija Sayi said...

Sasa hii ndio milo... nampa kila sifa mama yako..

Anonymous said...

Siku nikija kwako tafadhali, kisamvu cha karanga na wali vinahusika sana. Ngoja Cleo amalize kunyonya nitaianza diet kwa ukamilifu. Ila soda now nimepunguza sana wastani wa 15-21 kwa wiki now nipo kwenye 6-10 kwa wiki. Chai pia nakunywa ya asali na within 2 weeks nimepungua kutoka 67 hadi 65.

Interestedtips said...

Tina hongera sana mpenzi, umejitahidi, kuhusu kisamvu usija;i kipo sanaaaaaaaa

Da'mija thanx