Thursday, March 15, 2012

STATUS YA FACEBOOK ILIYONIFURAHISHA LEO

Hi!
Kuna thread moja inahusu michango ya harusi imenikumbusha mbali. Hivi

jamani, mnazijua gharama anazoingia bwana harusi hadi anapooa? Katika hali

ya kawaida kabisa, kama wewe ni mwanaume na unataka kuoa, jiandae kwa mambo

haya:

1. Kujitambulisha ukweni. Hapo utatakiwa uende kijijini alikozaliwa mkeo

mtarajiwa ukajitambulishe huko. Kama mfano mkeo anatokea Mwanza, na mnaishi

Dar, andaa nauli ya watu wawili, malazi kwa siku mbili, na utagharamia

shuhuli hiyo ya utambulisho. We tenga 500,000. Hapo tuna assume mkeo

atajitegemea. Otherwise 800,000 itakutoka.

2. Kumtambulisha mkeo kwenu. Kama nyie nyumbani ni Arusha, utatakiwa

umpeleke huko Ngarenanyuki. Sio umlete hapo Tabata mlipopanga. Hapo sio

kwenu! Andaa nauli yako na atakaekusindikiza, nauli ya binti na mwenzie, na

gharama za vinywaji na chakula siku hiyo. Utahitaji kama 700,000

3. Kifuatacho ITV ni kuwaalika wakwe zako nyumbani. Uwatoe watu kama nane

Mwanza, uwalete Arusha. Wale, walale, wajisaidie, kwa gharama zako. We acha
ubishi, tenga 800,000 tu.

4. Kwani we wazazi wako wanajua unakooa? Sasa je? Wasafirishe kwenda

Mwanza! Watu watano. Utahitaji kuwa na 500,000. Beba pia ATM card yako, kuna

imejensi.

5. MAHARI ndio topic inayofuata sasa. Ukiwa mjanja, unganishia kwenye

hiyo safari hapo juu uue ndege wawili. Pamoja na hayo, itabidi ubebe

2,000,000.

6. Sasa kijana unaweza kumvisha mchumba wako pete. Nunua ya kawaida

kabisa ya dhahabu. 350,000. Tukio lenyewe la kumvisha pete unaweza ita

marafiki wawili watatu ukatumia 200,000. Au fanya sherehe kabisa. Mi simo

7. Oke, sasa unaweza kuitisha vikao vya harusi. Tengeneza kadi za mwaliko

wa kamati kwa 200,000, kikao cha kwanza gharama zote ni juu yako. Andaa

500,000. Swali la kwanza kwenye kikao: "We una shing ngapi?" Sema 1,000,000.

8. Utahitaji 100,000 ya sms na simu kukumbushia michango. (Shukuru Mungu

kuna cheka time)

9. Wakati vikao vinaendelea, utatuma 200,000 kwa m-pesa ili mambo ya

kimila yaendelee kule nyumbani. We unaelewa

10. "Darling, sasa mi kwenye kitchen party ntavaa nini?" 300,000!

11. "Darling, kuna mahali nimeona gauni zuri la send." 400,000!

12. "Baby, rafiki yangu alinunua gauni la harusi China yani lilimpende..."

700,000!

13. Wakati huo wewe mwenyewe hujajua utavaa nini, hujanunua pete za

harusi, hujamvalisha best man na mkewe. Tuseme unahitaji kama 1,500,000

maana utalia lia sana. Kumbuka, gharama hizi huchangiwi na kamati. Wala
hutarudishiwa.

14. Siku ya send off lazma uende Mwanza. Utaenda mwenyewe? Ndugu wawili

watatu na mshenga 600,000. Kwenye send off utatakiwa kutoa sijui blanketi la

bibi, vitenge vya mashangazi, na vikorokoro kibao. Nunua hivyo vitu 300,000

uende navyo ili kupunguza gharama. Beba 200,000 za wale mashangazi

watakaoibuka ghafla!

15. Mshonee baba mkwe suti 100,000 mama mkwe yeye atavaa gauni la 50,000.

16. Fotokopi hiyo hapo juu (namba 15) kwa wazazi wako. 150,000
17. Watu watakaopenda kuvaa sare wajitegemee! Mimi sina hela! Ila
utavishonea nguo vile vitoto kwa 80,000.

18. Siku mbili kabla ya harusi, utaanza kupokea wageni. Unatakiwa

uwatafutie malazi na chakula. Kwa ujumla utahitaji kama 500,000

19. Jioni watoe auti mashemeji zako ambao hawajawahi kufika Dar

ukawanunulie bia ili wakuone wa maana. 200,000

20. Siku ya harusi bibi harusi na mwenzie na watoto na ma maids watatakiwa

wakapambwe saluni. 200,000

21. We na mwenzio mtaenda kunyoa hapo kwa nanii. Ndevu na nywele na black

kibishi 40,000

22. Siku ya harusi beba sadaka 10,000. Wakati huo umeshamtuma kijana

akakulipie hoteli mtakayofikia baada ya harusi. Kamati haitoi hela hiyo, so

utalipa malazi ya siku mbili 200,000

23. Kama mtaenda honeymoon sehemu yoyote nzuri nzuri nje ya mji, si chini

ya 800,000 kwa angalau siku 5.
24. Wakati uko huko honeymoon, huna hata kumi, mwanakamati mmoja ambae
hakuchanga anakupigia simu " Sasa tunavunja lini kamati?" Pesa yote

iliyochangwa ilitumika kwenye harusi, sasa gharama za kuvunja kamati ni za

nani?? 500,000!

25. SASA MNAANZA MAISHA YA UNYUMBA. 14,180,000 poorer.

 
KAZI KWENU MSIOOA/MTAKAOOA TENA.KAM VIPI JIWEKE MAPEMA HAAA HAAAAAA HAAAAAA
 
FROM MARGATETH BEREGE FACEBOOK PAGE

1 comment:

Anonymous said...

Thank you so much! This a wonderful website!