Friday, March 9, 2012

PIKI PIKI NA AJALI ZA KILA SIKU


Dereva wa piki piki anatakiwa awe katika mazingira gani ili awe salama awapo barabarani, abiria wake aweje pia? Leo nimeona tulizungumzie swala hili kwani ajali zinaongezeka kila siku, hospitali nyingi siku hizi idadi ya majeruhi hasa wa piki piki inaongezeka
Kituo cha Boda boda, madereva wengi hapo wanaonekana hawana Helmet, na ni kosa kuendesha bila kuwa nayo kwani ni hatari kwa afya yako. Mteja pia anapaswa avae kwani mkipata ajali wote mnaanguka na atleast zinaprotect kuliko kuto kuwa nazo kabisa

Mdada na Helmet yake, wadau je! hapo mwilini mnasemaje bila kuwa na Jacket?

Mishikaki Style, Dereva peke yake ndo ana Helmet, abiria wake tena wawili hawana, je!ni sheria kubebana namna hii? au kwakuwa tunajua kusingizia usafiri ni wa shida ndo maana tunabebana hivi? Hatuwazi  madhara yake, leo mguu umetoka,kesho sikio hakuna,la hasha sio kwamba nataka ajali, ila ni tahadhari tu

Na inasemekana asilimia kubwa ya madereva wa piki piki hawazijui sheria za bara barani, wanachojua ni kufundishana wenyewe, ajue kunyoosha then atafute piki piki ilipo na Leseni, aanze mzigo, hawazi kama kuna ajali na madhara mengine, ndo maana hawaoni umuhimu wa Helmet wala Jacket na kutozingatia sheria za bara barani

Jacket huwa zinawasaidia kuprotect upepo unaowapuliza kwa speed kwani wanakuwa kama wanapingana nao, kuna kudhurika kifua, vichomi kupata, lakini wao hawawazi hayo wanaona poa tu

Watu wa piki piki tuoneeni huruma jamani, piki piki zinatuharakishia sana katika ratiba zetu, naamini wapo wanaojali sheria nawapa hongera sana, leo nazungumzia walio wazembe na kusabaisha vifo kwa Raia

Piki piki mpya imetoka dukani, hii nina imani inaenda kuwa boda boda, ukawe chombo kizuri uendako, dereva wako akakutunze na atunze abiria watakao kupanda, hakuna apendaye ajali wala kufa, inatokea kwa uzembe wetu tu mwingine

Kama ajali hii jamani hadi huruma


Mimi naamini atleast huu ni uvaaji mzuri wa dereva wa Piki piki, sasa hapa uwe na leseni yako halafu sheria za bara barani uzijue vizuri, utafurahia udereva wako
N.B. Hayo niliyoyaeleza hapo juu ni mawazo yangu na uelewa wangu, kwani juzi niliumia sana kuna mtu namfahamu kapata ajali ya piki piki kavunjika kiuno, mwenye lolote la kushare karibu sana niandikie ester.ulaya@gmail.com

2 comments:

ngaizaskids said...

Nachukia pikipiki yaani Mungu anajua, Uganda zinapitapita mpaka unakasirika nazo, czipendagi kwa kweli zinakera. Sijui kwa nn walizipitisha Bk zilikuwa haziruhusiwi yaani zinachafua mji. Na nihatari, bila jacket ni kujinywesha sumu mwenyewe.

Ester Ulaya said...

Mimi naziogopa hadi basi jamani, mwenzetu kavunjika kiuno kwasababu ya piki piki, nimeshuhudia ajali nyingi za piki piki, sizipendi kabisa