Saturday, February 4, 2012

Food Preservation

Kuna namna nyingi ya kuhifadhi mazao, lakini kila mila ina namna yake...picha hii inamuonyesha mama wa kijiji cha Kangeme-Tabora akiandaa Chakula kwaajili ya matumizi ya sasa na baadae. Katika ukanda wa kanda ya ziwa hususan mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Tabora hasa vijijini wakazi wao huhifadhi mazao kwa njia ya kuanika juani katika vichanja, lengo la kuweka katika vichanja ni yasibunguliwe na wadudu, maana huwa yanakuwa nje kwa muda mrefu hasa kipindi cha kiangazi huku yakiliwa/kuuzwa taratibu hadi kipindi cha Masika kifike. Njia hiyo ya kuweka katika vichanja na kuanika mazao hayo huwa ni ya ki-mila kama picha za chini zinavyoeleza.  Na wanapofanya hivyo mazao huwa katika hali ya usalama zaidi wakati wote.
Kihenge cha Mahindi ambapo yanaonekana kuhifadhiwa taratibu kadiri yanavyokauka

Hii ni michembe, ambayo hutokana na viazi vitamu vinakatwa vipande vidogo vidogo na baadae kuanikwa juani
Matoborwa, hutokana na viazi vitamu vinavyochemshwa na baadae kukatwa katwa vipande vidogo vidogo, halafu vinaanikwa juani

Hizi ni Nyanya, zinakatwa katwa halafu zinaanikwa juani,ambazo hutumika kwenye mboga

Makopa; ni mihogo ambayo inavundikwa halafu inaanikwa juani.

Mpenzi msomaji hii yote hutokana na ukosefu wa vitu kama Fridge, Dawa za kuweka ktk mazao ili yasibunguliwe, masoko kuwa adimu hivyo mazao yasiharibike na kutupwa.

1 comment:

Mija Shija Sayi said...

Mapalage na matoborwa ni matamu balaa..