Wednesday, August 27, 2014

DIAMOND NA DABO WATAJWA KUWANIA TUZO ZA 'IRAWMA', MAREKANI


Wasanii wa Tanzania,  Diamond Platinumz na Dabo (wa Dancehall) wametajwa kuwania tuzo za IRAMWA (International Reggae and World Music Awards), Marekani.
 
Wimbo wa MdogoMdogo wa Diamond umemuwezesha kutajwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha The Best African Song/Entertainer akichuana na Davido (Aye), Awilo Longomba (Bendeke), Willy Paul Msafi (Tam Tam), Eddy Kenzo (Sittya Loss), na Bracket (Mama Afrika).
 
Naye msanii wa dancehall, Dabo ametajwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha Best New Entertainer.

Upigaji kura tayari umeshafunguliwa na tuzo hizo zitatolewa October 4 nchini Marekani.
 
Wapigie kura wasanii hawa wa nyumbani ili kuwawezesha kuleta ushindi nyumbani. Ingia www.irawma.com na uchague vipengele wanavyoshindania.

No comments: