Monday, August 27, 2012

JANA NILIHESABIWA.........SENSA 2012

 Jana nimekaa ndani hadi saa 11 jioni wana sensa hawajapita...ile natoka ndani tu nimefunga mlango nikafanye mizunguko, naona Karani anaingia
 Ikabidi nihesabiwe nikiwa nimesimama hapo hapo nje...na karani hakuwa na hiyana
 Nikaanza kuhojiwa...nikatoa ushirikiano woteee
 Alikuwa anatik kila nikimjibu swali
Hapa alikuwa ananiambia dodoso langu lina maswali 37...wapo ambao wana wanaulizwa maswali hadi 60

Kwa wale ambao hamjahesabiwa....mtahesabiwa tu, ndo maana kuna siku 7

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Duh! nitawahi kweli kuhesabiwa na mimi?:-(

emu-three said...

Hongera mpendwa, tumekuongeza kwenye kura yetu 2015, ww usifike kupiga kura, umeshapiga tayari!

Ester Ulaya said...

asanteni sana...dada Yasinta sidhani kama utawahi

R.Ngaiza said...

Nasikitika nimepitwa lol! Maswali 60 si kichwa kitauma inamaana majibu ya maswali mengine wanayo huko serikalini ndiyo maana ukapatiwa kidogo. Heri umemaliza sasa uswampe vizuri my wii wangu Kizuri.