Saturday, April 7, 2012

R.I.P STEVEN KANUMBA


Mashabiki wakiwa wamekusanyika katika viunga vya hospitali ya Muhimbili. Habari za awali ambazo kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni Afande Kenyela amesema kuwa Kanumba alikuwa na kutoelewana kati yake na Mpenzi wake ambazo taarifa za awali zinasema waligombana na Kanumba alisukumwa na kugonga kichwa chini na mpenzi wake ambaye ametambuliwa kwa jina moja la Lulu.

Habari ambazo bado Spoti na Starehe haijazithibitisha zinasema kuwa Kanumba alikuwa akioga ili atoke na ndipo aliposikia mpenzi wake akiongea na simu na mtu mwingine alipotoka kumuuliza ndipo mzozo kati yao ukaanza na katika hali ya kusumunana Kanumba alisukumwa akaanguka na kugonga kichwa chini.

Afande Kenyela alisema alipigiwa simu na ndugu wa Kanumba ambaye walikuwa wakiishi pamoja na Kanumba na walipofika Pale walikuta tayari ameshakata roho ila bado inasubiriwa ripoti ya daktari.

Kamanda Kenyela pia amesema kuwa mpenzi wake Maerehemu Kanumba anashikiliwa na Polisi kwa uchunguzi zaidi. Lulu ambaye naye anag’aa kwenye tasnia ya Filamu amekuwa akigonga vichwa vya habari vya magazeti ya “udaku” kutokana na skendo za mara kwa mara za mahusiano ya kimapenzi, ni majuzi tu mwanadada huyu ametimiza miaka 18 tangu kuzaliwa.

Aidha nyumbani kwa marehemu Sinza kumejaa ndugu jamaa na marafiki kiasi barabara ya kwenda Lion kupitia Madukani inapitika kwa taabu.

Kanumba ambaye alizaliwa mwaka 1984 amefanikiwa kuzikonga nyoyo za mashabiki wa tasnia ya movie za Tanzania si tu kwa Tanzania bali hata nje ya nchi pia.

Kwa mashabiki wa filamu za kibongo Kanumba alikuwa ni namba moja na kwa kiasi kikubwa aliweza kuweka viwango kwani alikuwa anafaa kwa kila kona kuanzia kuigiza mpaka kuvaa na adamu ya maisha tofauti na ma Super Star wengine hivyo kuwavutia watu wa rika lote.

Pia ndiye aliyewatoa watu kama Akina Wema Sepetu, Mtoto Sophia ambaye aliigiza kwenye Movie ya Big Daddy, pia ndiye aliyemtoa Patchou Mwamba na kumuingiza kwenye Movie Industry. Kanumba anamaliza kipindi chake cha miaka 28 akiwa ameacha kumbukumbu ambayo itaishi kwa muda mrefu.

Mashabiki kupitia mitandao ya kijamii wameonyesha masikitiko yao ambapo kufika saa tisa usiku habari zilikuwa zikisambaa kama moto nyikani kupitia Facebook, Twitter na Blogs ikiwemo hii ya Spoti na Starehe ambayo ilikuwa moja ya wa kwanza kupata habari.

Picha/ Habari: Shamim Mwasha, Sport Starehe.

No comments: