Wednesday, March 28, 2012

STATUS ILIYONIKUNA FB - UNAWEZA UA WAZAZI KISA HOME WORK

Baba na mama, ni matumaini yangu kuwa mtasoma ujumbe wangu huu kwenye karatasi niliyoiweka juu ya meza,naomba msishtuke mana ni mambo ya kawaida kwenye maisha tunayoishi, najua mtaumia kwa vile bado nasoma
na ndo nipo kidato cha kwanza,

Napenda kuwajulisha kwamba sasa hivi mnaposoma hii barua sipo nyumbani,nimetoroka mana nimegundua nina uwezo wa kujitegemea kwa sababu mi ni kijana mwenyewe umri ...wa miaka 14 na ninajua kipi chema na kipi kibaya. tangu mwezi mmoja uliopita nilikuwa na uhusiano na binti mmoja aliyeitwa Rachel, mwenye umri wa miaka 27 na kwa sasa ndo naishi naye kwenye chumba alichopanga.

Nilipokuwa nyumbani sikuwa napata hela za kutosha ila sasa nimeanza kushika noti za shilingi 10,000, msichana niliyenaye ni mzuri sana wa umbo na ninampenda sana,amenifundisha njia za kutafuta hela.

Amenipangia kazi ya kuuza madawa ya kulevya na yeye ikifika usiku anaenda kuuza mwili wake, basi kila siku tunapata hela ya kutosha,huyu mchumba wangu ni msichana mwenye bidii,kwa siku analala masaa 6 tu maana mwanaume yeyote akija lazima awe naye chumbani kwa mda wa masaa 3.Msiwe na hofu,nipo salama kabisa na nimeamua kumwoa Rachel mana ni kila kitu kwangu.

Pia amenunua gari la kubebea mbao kwahiyo biashara inaenda vizuri,Rachel ameenda kupima afya na amekutwa na upungufu wa kinga mwilini, mara nyingi namridhisha anapotaka kitu flani,iwe kufanya naye mazoezi ya viungo au kufanya naye mapenzi, si mnajua unapokuwa na mgonjwa unakuwa naye karibu, ila mi pia sijihisi vizuri mana kila saa nakohoa tu na sina uhakika kama nimeathirika,.

Tumepanga baada ya miaka miwili tutawatembelea,nadhani mpaka miaka miwili iishe atakuwa ameshajifungua,na nifuraha yangu mtamwona mjukuu wenu.Wazazi wangu sina la kuongeza kwaherini Mungu akipenda tutaonana.

Baba na mama mi nipo chumbani kwangu, mnachokisoma ni h/work ya mwalimu wa kiswahili alituambia tutunge hadithi fupi,naomba iangalieni kama kuna makosa

2 comments:

kokusimah said...

Du! Aisee hii ni nouma nimestujaje roho ya gazeti mie, juu dogo.

Interestedtips said...

yaani dogo atakuwa alipata maksi za nguvu, anajua kuandika huyooooooooo