Sunday, February 12, 2012

PISHI LA LEO - TEMBELE

Leo tutaongelea upikaji wa Matembele, ambayo yanapikwa na mwananchi wa kawaida kabisa
Ananunua fungu La Tembele shilingi 200/-, Nyanya 300/-, Kitunguu 100/-, Carrot 200/- akitaka/akipenda na Hoho 200/- bila kusahau kibaba cha mafuta ya kula
Akajitwalia mafungu mawili yaliyoshiba
Unayachambua vizuri, halafu unayaweka juani yanyauke kiasi
Ukiridhika na unyaukaji wake, yasafishe vizuri na maji uhakikishe mchanga umetoka
Andaa viungo vyako, kwa mimi sikupenda kuweka hoho, hivyo nikaandaa, Kitunguu,Nyanya na Carrot, pia haishauriwi kutumia nyanya nyingi kwenye mboga, zina Acid, zaweza kusababisha madhara tumboni hasa vidonda
Weka kijiko/vijiko cha mafuta sufuriani hapo itategemea na wingi wa mboga uliyonayo, mafuta mengi si mazuri kwa afya, mafuta yakipata moto weka vitunguu vilivyo katwa katwa, uwe unageuza geuza hadi viwe na rangi ya kahawia
Vitunguu vikiwa na rangi ya kahawia, weka nyanya zako ulizo kata kata, geuza geuza, uweka Carrot ulizo katakata, geuza geuza ili mchanganyiko uwe sawa, kama una hoho ulizo kata kata weka pia, pima kiwango cha chumvi weka, endelea kugeuza geuza hadi mchanganyiko ulainike vizuri na uridhike, usitumie muda mrefu sana kuepuka kukauka
Ukisharidhika weka Matembele yako kwenye ule mchanganyiko, geuza geuza, halafu funika, kama kawaida mboga za majani hazitakiwi kuiva sana ili kuhifadhi vitamini vyake vifae mwilini kiafya zaidi, ndani ya dakika 5 hadi 7 funua uangalie mboga yako uigeuze geuze kidogo, waweza onja chumvi na kama imeiva, ipua
Hapa mboga yetu iko tayari kuliwa
Waweza kula na ugali, wali, mihogo ya kuchemsha, viazi vya kuchemsha nk.
Enjoy your Meal

Tembelea hapa ujifunze mambo mengi kuhusu afya yako 

6 comments:

lipoooo said...

very intresting blog with nice pictures! :) I really like it :)

Interestedtips said...

Thanx Lipoooo

kokusimah said...

Du dear sikujua kuwa tembele si mboga ya kukimbilia kwa hiyo km nvua imenyesha ugali naurumangia chumvi? Asante kwa kusomo Bukoba hatuna utaratibu wa kuyala ndo unaingia. Sasa dear huku wanauza yalosagwa Kama kisanvu nakugandishwa kwenye jokofu, je mwendo ni huu huu au?? Niliwahi kuyanunua niyajaribishe nkachemka. Nambie mwisho wa mwezi nkajaribu tena Kama pishi hili linaenda nayo. Keep it up mama. Pamoja.

Interestedtips said...

My dear, mara nyingi yaliyotengenezwa kama kisamvu nayo mwendo ni huo huo, kwa jinsi nifahamuvyo mie, mwenye ujuzi mwingine namna ya kupika atujuze ili tuongeze ujuzi zaidi

kokusimah said...

Ntayamendea huko kwa mhindi nikiyakuta nayapeleka mwendo huu alafu ntakupa majibu. Asante kwa kujibu.

brizzleleo.blogspot.com said...

bonge lapishi jamani.nimemiss matembele sana