Friday, February 17, 2012

HOW WAS YOUR VALENTINE'S DAY?

Tarehe 14/02/2012 hii siku ilikuwa ngumu kidogo kwangu, kwani tokea saa 3 asubuhi nilikuwa Muhimbili National Hospital, hapo nilikutana na watu wa kila aina, wagonjwa, wauguzi na wananchi mbali mbali waliokuwa wameenda kutembelea ndugu na jamaa zao na nilifanikiwa kupata rafiki mpya ambaye ninawasiliana naye hadi leo
 Wagonjwa wakiwa ktk viti wakisubiri kuingia kwa Daktari wapate huduma ya Afya, maana Afya kwanza ndo mambo mengine yanaweza songa mbele
 Muuguzi
 Kadiri muda ulivyokuwa ukisogea mabenchi ya kukaa wagonjwa yalizidi kujaa, no more mgomo nenda kahudumiwe na utahudumiwa
Wauguzi walikuwa busy kweli, mara waingie humu, watoke waende huku, yote hayo ni kuhakikisha huduma zinatolewa kwa walengwa
 Mavazi yao niliyafurahia, Makoti meupeeeeeeeeeee, masafiiiiiiiiiiii na Vazi la Gauni likiwa poa sana, kama huyu Dk. Nilipenda uvaaji wake
Muda wa kupata Lunch uliwadia, na misosi tuliishambulia sana, hapo ni moja wapo ya Canteen ya Muhimbili
 
 Late hours ndo nikawa naingia ndani, nafika tu nakutana na Ua mezani, likinukia hasa, siku ikawa imeisha vizuri sanaaaaaaaa
Je! wewe ya kwako mdau ilikuwaje?

No comments: