Wednesday, March 7, 2012

TUZUNGUMZE KUHUSU AFYA SIKU YA LEO

Siku ya leo napenda tukumbushane juu ya kuzingatia afya zetu, hasa mara tu, tuamkapo asubuhi na tunavyoshinda mchana hadi jioni. Kuna ambao wakiamka jambo la kwanza anajinyoosha viungo, kuna wanaofanya mazoezi, kuna wanaoamka na kuanza shughuli za nyumbani, kuna wanaoamka na kuoga wakijiandaa kwenda kazini. Kutokana na Ushauri mbalimbali kutoka kwa Madaktari, wengi wanashauri yafanyike mambo 7 pindi unapoamka tu kitandani na jinsi uishi siku nzima. Lengo ni ku maintain afya zetu na kuzifanya ziwe imara siku zote, na ukizingatia hayo waweza ishi miaka 20 ijayo ukiwa hivyo ulivyo sasa au ukawa bora zaidi ya leo

1. Pindi uamkapo kitandani, taratibu vuta hewa ndani kwa muda wa sekunde 2 hadi 3, halafu uitoe nje taratibu. Rudia mara 2 hadi 3. Deep breath Huwa inasaidia kupunguza stress na kukufanya utulie, inaongeza oxygen kwenye damu, .
 Ukilala Chali ni rahisi sana kufanya zoezi la kuvuta na kutoa hewa
 Waweza kwenda nje kwenye hewa/oxygen nyingi ukafanya zoezi hilo
2. Kunywa maji walau Glass 1 hadi 4 baada ya ukamaliza zoezi namba 1, waweza kunywa chai baada ya dakika 45.
 Maji yana kazi nyingi sana mwilini. Yanasaidia kuwa na nguvu sana mwilini, kuondoa uchovu, yanasaidia kupunguza uzito, ngozi haiwi kavu,n.k

3. Kula vizuri, balanced Diet. Inatakiwa ule vyakula vyenye (a) Wanga ambavyo huleta nguvu mwilini, (b) Protein ambavyo husababisha ukuaji na repair (c) Fat vyakula vyenye mafuta pia ni chanzo cha nguvu mwilini (d) Vitamins: these are required in very small quantities to keep you healthy (e)Mineral salt inatakiwa sana kwa ajili ya meno,mifupa, misuli nk.
4. Fanya mazoezi. Yanapunguza uwezo wa kupata magonjwa ya Moyo, they reduce the risk of developing high cholesterol, ni mazuri kwa wafanyao diet, yana strengthen immune system nk.
5. Kujicontrol, hasa kila kitu kwa kiasi.Unywaji wa kiasi, Ulaji kwa kiasi, Kujig jig kwa kiasi nk.
6. Ishi kwa matumaini, kwa chochote kile hasa kwa afya
7. Kupumzika zaidi ya masaa 6 ni vizuri kwa afya
Kulala zaidi ya masaa 6, hasa yawe masaa 7-8 ni afya zaidi, inapunguza magonjwa ya moyo,inaondoa uchovu,uwezo wa kufikiri unaongezeka nk.  Tena watoto wanatakiwa walale masaa mengi zaidi kwakuwa bado wanakua

Kwa uchache pokeeni hayo niliyoyaandaa, naamini ukiyafuatilia kwa ukaribu yatakusaidia, afya ni muhimu sana
Kama una lolote kuhusu hili au lingine unapenda kushauri au kuongezea na kututumia mapya, usisite kutuandikia ester.ulaya@gmail.com
Nawapenda sana wadau wangu, karibuni tena na tena

No comments: