Showing posts with label Kumbu kumbu. Show all posts
Showing posts with label Kumbu kumbu. Show all posts

Friday, August 31, 2012

JUZI NILIKATIZA MITAA AMBAYO INANIKUMBUSHA UKOMAVU WANGU WA MAISHA YA KUJITEGEMEA ULIANZAJE

 Experience tuipatayo wakati ndo unaanza maisha ya kujitegemea kila mtu anaijua yeye mwenyewe
 Hasa ndo umetoka Shule/Chuo unasema sasa naanza maisha yangu....unajipangia kila kitu wewe mwenyewe
 Niliwahi kuishi mitaa hii wakati ndo nimeanza maisha..........baada ya kumaliza chuo
 Huo mshale mweusi unpoelekeza ndo kona ya kuelekea nilipokuwa nimepanga
 Enzi hizo palikuwa hakuna Rami kabisaaa...ni mwananyamala kwa kopa......juzi nilipita nikapakumbuka sana
 Nilipata taswira ya mambo yaliyokuwa yakiendelea mtaani huko
 Kwanza huo mtaro unaouona umejengwa kipindi hicho ulikuwa haujajengwa, palikuwa ni vumbi na magari yalikuwa yanapiata hapo.....kasheshe ilikuwa mvua ikinyesha...siku hiyo siendi job...nitajitahidi niwaambie naumwa...yaani maji yalikuwa yanajaa...halafu hayaeleweki yana kila rangi, nilikuwa nalala tu...ikinyesha mfululizo nakumbuka nilikuwa na maviatu yangu makubwaaaa nayavaa walau niwe juu juu maji yasinipate, nikifika job nabadilisha...uzuri ofisi ilikuwa jirani na home kwa kutembea ni 5-10 minutes
Hapo ukiingia kulia baada ya hako kauchochoro ndo kuna nyumba niliyokuwa naishi...pichani haionekani......Zilikuwa zinapigwa taarabu ni balaaa.....karibia kila nyumba halafu sauti kubwaaaa...sijui walikuwa wanatambiana....yaani nikikumbuka nacheka mwenyewe...uzuri wa magenge ya huku nilikuwa naaford sana bei zao...unakuta nyanya fungu hadi shiling 100 unapata, vitunguu vitatu vidogodogo shilingi 50, maisha yalikuwa Cheap.....Kodi nakumbuka kwa mwaka nililipaga 180,000/- ila nilikaa miezi 11 nikahama.....sasa nyuma ya dirisha palikuwa ni kituo cha wavuta ganja, humo ndani kizungu zungu kilikuwa kinanikoma.....ikabidi tu nihame.......ukweli huwa nakumbuka mambo mengi sanaaaaa.......halafu nacheka, nafurahi kuwa ndo ulikuwa msingi wangu wa kuanza kujitegemea na kupanga maisha yangu yaweje...........KWA MIMI NI KUMBU KUMBU NZURI SANA